April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Maalim Seif arejea nyumbani kwake

Spread the love

MAALIM Seif Sharif Hamad, mshauri mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, aliondoka kwenye Kongamano la Kuadhimisha Miaka 9 ya Maridhiano visiani humo na kurejea nyumbani kwake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa za awali zilieleza, mwanasiasa huyo mkongwe na mwiba kwa Serikali ya Rais Mohammed Shein na Chama Cha Mapinduzi (CCM) visiwani humo, alikwenda polisi kuitikia wito.

Ni baada ya ujumbe wa Jeshi la Polisi kumtaka aende kwa ajili ya mahojiano. Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuondoka kwenye kongamano hilo, Maalim Seif alikwenda moja kwa moja nyumbani kwake.

Kwenye kongamano hilo, Maalim Seif aliondoka huku akisindikizwa na baadhi ya polisi jambo ambalo liliashiria kwenda kuitikia wito huo.

Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Pili wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), alihudhuria konagamano hilo lililoandaliwa na Mzee Nassoro Moyo, mwanasiasa mkongwe visiwani humo.

Kongamano hilo lilisimamishwa saa 6 mchana kwa agizo la Jeshi la Polisi. Hata hivyo, polisi walidai muda wa kongamano hilo ulikwisha.

error: Content is protected !!