Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo TFF yathibitisha Tanzania kupeleka timu nne CAF
MichezoTangulizi

TFF yathibitisha Tanzania kupeleka timu nne CAF

Ofisi za TFF
Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limethibitisha kuwa msimu ujao wa mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF), Tanzania ni moja ya nchi itakayoingiza timu nne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye shirikisho hilo, imesema kuwa, timu hizo zitashiriki kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo zitaenda timu mbili, na michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambapo kutakuwa na timu mbili pia.

Nasafi hizo zimepatikana mara baada ya Tanzania, kuwa moja ya timu zilizokusanya pointi nyingi kwenye michuano ya CAF katika misimu ya hivi karibuni.

Michuano hiyo kwa msimu ujao wa mashindano 2021/22, itaanza kati ya tarehe 10-12 Septemba 2021 na marudiano itakuwa kati ya tarehe 17-19 Septemba 2021.

Mara baada ya michezo hiyo ya awali, hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika, itachezwa tarehe 11-13 Februari 2022.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kupeleka timu nne kwenye michuano ya CAF, mara baada ya kufanya hivyo kwenye msimu wa 2019/20.

Katika msimu huo, timu nne zilizowakilisha nchi zilikuwa Simba na Yanga ambao wao walicheza michezo ya Ligi ya Mabingwa, huku KMC na Azam FC walishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

error: Content is protected !!