March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yamfungia Kuuli kutojihusisha na soka

Wakili Revocutus Kuuli

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kamati ya maadili imemfungia maisha kujihusisha na soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocutus Kuuli baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ya kimaadili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Makosa hayo ambayo ni kusambaza nyaraka za TFF kwa watu ambao haziwahusu ambapo ni kinyume na utaratibu wa taasisi hiyo, kutoa maelezo yanayoonesha kuwa na mgangano wa kimaslahi na kufanya vitendo vinavyopelekea kulishusha hadhi shirikisho hilo.

Akisoka uwamuzi huo Mwenyekiti wa kamati ya maadili kwenye shirikisho hilo Wakili Hamidu Mbwezeleni ameeleza kuwa makosa hayo yote matatu yanastahili adhabu hiyo ya kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu na hakuna aliyeonewa.

“Uamuzi huu umechukuliwa kwa kufuata kanuni na taratibu. Hakuna aliyemuonea Kuuli niliweke hilo sawa,” alisema Wakili Mbwezeleni.

Ikumbukwe Kuuli alijiuzuru nafasi hiyo ikiwa siku chache baada ya katibu Mkuu wa Tff Wilfred Kidao kumwandikia barua ya kujieleza ndani ya siku tatu kwanini alisimamisha uchaguzi wa klabu ya Simba.

error: Content is protected !!