Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Michezo Diamond azindua Wasafi Festival, amwita Ali Kiba
Michezo

Diamond azindua Wasafi Festival, amwita Ali Kiba

Spread the love

MKURUGENZI mkuu wa kampuni ya Wasafi Naseeb Abdul maarufu kama ‘Diamond Platnumz’ ametangaza ujio wa tamasha kubwa la burudani Wasafi Festival ambalo linatarajia kuanzia mkoani Mtwara 24 Novemba, 2018 na kuzunguza katika baadhi ya mikoa nchini na kuelekea mpaka n je ya nchi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya ‘Mchezo usiuchezee wewe Kabisa’ litafanyika mkoani Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, na baadae kwenda mkoani Iringa na Morogoro na baadae kwenda kufanyika nchini Kenya katika jiji la Nairobi 31 Novemba Mwaka huu.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Diamond alisema kuwa mbali na burudani ujio wa tamasha hili utakwenda sambamba na kusaidia jamii katika mkoa husika kama kutoa mitaji kwa wakina Mama 200 pamoja na kusaidia wanafunzi.

“Tunataka tamasha hili kila linapofika liwanufaishe wakazi wa pale siyo kwenda tu kuchukua hela zao na kusepa, na kwa kuanzia tutawasaidia kina mama,” alisema Diamond.

Sambamba na hayo Diamond aliongezea kuwa tamasha hilo litajumuisha wasanii wote wanaofanya vizuri nchini kwa sasa na huku akitamani hata msanii mwenake ambaye anaonekana kuwa mpinzani wake mkubwa katika kazi zao za muziki Ali Kiba naye akiwepo.

“Natamani kaka yangu Ali Kiba naye awepo na ninaamini uongozi wangu utaanza mazungumzo naye na huko alipo kama anafuatilia wasafi ajue tungehitaji uwepo wake, kwani inabidi tutoke kwenye muziki wa mabifu na tuingie katika kutengeneza hela na kuisaidia jamii inayotuzunguka,” aliongeza Diamond.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Michezo

Unamalizaje Jumapili hujabeti na Meridianbet?

Spread the love JUMAPILI ya leo tutashuhudia mitanange kibao ambayo itamalizika kuanzia...

Michezo

Jipigie pesa na Meridianbet leo hii

Spread the love KAMPUNI kubwa ya ubashiri Tanzania inakwambia hivi huu ndio...

Michezo

Endelea kubashiri na Meridianbet, Ligi bado zipo

Spread the love BAADA ya ligi mbalimbali kutamatika, bado kuna ligi mbalimbali...

error: Content is protected !!