March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Ndugulile amweka ndani Mganga Mkuu

Spread the love

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile ameagiza Jeshi la Polisi wilayani Mbulu mkoa wa Manyara, kuwaweka ndani Mganga Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Joseph Foma na Mhandisi wa ujenzi wa kituo cha afya, Mhandisi Samweli Bundala. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dk. Ndugulile ameagiza mganga huyo kuwekwa ndani baada ya kukagua ujenzi huo na kubaini mapungufu ya kitaalam katika ujenzi wa kituo hicho kilichopo kata ya Dongobeshi wilayani Mbulu.

Katika ukaguzi huo, Dk. Ndugulile alibaini madudu katika kituo hicho, kwa kukuta makosa ya kiufundi kwenye eneo la upasuaji na sehemu ya kuifadhi maiti.

‘’Kamanda mkuu wilaya weka ndani wote wawili akili iwakae sawa inakuwaje mhandisi unakaa eneo la ujenzi bila kuwa na ramani ya ujenzi na mganga mkuu unashindwa kutoa ushauri kwa wataalamu wa ujenzi kujenga kituo cha afya bila kuzingatia vigezo vya kitaaluma katika ujenzi wa eneo la upasuaji,” alisema Dk. Ndugulile.

error: Content is protected !!