Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Michezo TFF yaja na Bonanza la Waandishi
Michezo

TFF yaja na Bonanza la Waandishi

Boniface Wambura, Mkuu wa Habari na Masoko wa TFF
Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa bonanza kwa ajili ya vyombo vya Habari litakalofanyika tarehe 6 Desemba 2020 kwenye viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kewlvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Bonaza hilo ambalo litajulikana kwa jina la TFF Media Day likiwa na lengo la kukutanisha waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini na kujumuika pamoja katika kuumaliza mwaka.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura amesema lengo la bonaza hilo ni kutambua na kuthamini mchango wa vyombo vya habari kataka maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

“Vyombo vya habari ni moja ya wadau wetu wakubwa katika kutangaza na kufahamisha wadau wa mpira wa miguu kuhusu TFF, nini tunataka kufanya na pia tutatumia muda huo kukutana na waandishi pamoja na viongozi wa TFF nje ya maeneo ya kazi,” alisema Wambura.

Aidha Wambura aliongezea, Bonanza hilo halitaishia mwaka huu bali litakuwa ni tukio litakalofanyika kila mwaka ila huu utakuwa ni mwanzo tu.

Jambo hili litakuwa ni mara ya kwanza kwa Taasisi hiyo ya juu kwenye mpira wa miguu nchini kuandaa siku kwa ajili ya vyombo vya habari ambayo itakuwa inashirikisha michezo mbalimbali huku lengo likiwa ni kufahamia Zaidi nje ya mazingira ya kazi.

Bonanza hilo ambalo litaanza majira ya saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni litakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mziki pamoja na mchezo wa kuvuta kamba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

TANROADS wawataka watumishi wazingatie michezo kazini

Spread the love  WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imesema michezo inapaswa kuzingatiwa...

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

error: Content is protected !!