Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Majaliwa: Vifo vinavyotokana na Ukimwi vimepungua
Habari za Siasa

Waziri Majaliwa: Vifo vinavyotokana na Ukimwi vimepungua

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu,
Spread the love

VIFO vitokanavyo na Virusi Vya Ukimwi (VVU), vimepungua kutokana na uimarishaji wa huduma za tiba ikiwemo matumizi ya dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARVs). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu leo tarehe 1 Desemba 2020, katika maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Mandela, Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema, matumizi ya ARVs kwa kiwango kikubwa yamechangia kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI kutoka vifo 85,000 mwaka 2001 hadi kufikia vifo 21,529 mwaka 2019.

Waziri Majaliwa amesema, mbali na kupungua vifo hivyo, pia maambukizi mapya ya UKIMWI yamezidi kupungua kutoka watu 130,000 mwaka 2001 hadi watu 68,484 mwaka 2019.

“Mafanikio yote haya yametokana na kuendelea kuimarika kwa huduma za tiba ikiwemo matumizi ya dawa za kufubaza VVU (ARVs), pia afua za kinga zinazohusisha tohara ya kitabibu kwa wanaume na kuzuia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto,” amesema.

Amesema, Tanzania imefanikiwa kufikia malengo ya tisini tatu (90:90:90) hasa katika 90 ya pili na ya tatu. “Kwa kujikumbusha tu, ni kwamba tisini tatu zinalenga kuhakikisha kuwa asilimia 90 ya WAVIU wanajua hali zao; asilimia 90 ya wanaojua hali zao wanaanza kutumia dawa za kufubaza mapema na asilimia 90 ya walioanza dawa za kufubaza VVU kinga zao za mwili zinaimarika ifikapo mwaka 2023.”

Pia Waziri Majaliwa ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wadau mbalimbali wa masuala ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI, waongeze jitihada hususani katika kuhamasisha upimaji wa VVU ili wafikie lengo la 90 ya kwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaTangulizi

Mapya yaibuka wamasai waliohamishwa Ngorongoro kwenda Msomera

Spread the loveMAPYA yameibuka kuhusu zoezi la Serikali kuwahamisha kwa hiari wamasai...

Habari za Siasa

Rais Samia ampongeza mpinzani aliyeshinda urais Senegal

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mwanasiasa wa...

Habari za Siasa

Ushindi wa mpinzani Senegal wakoleza moto kwa wapinzani Tanzania

Spread the loveUSHINDI wa aliyekuwa mgombea  urais wa upinzani nchini Senegal, Bassirou...

error: Content is protected !!