Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee atoa sharti Chadema kutema ubunge
Habari za Siasa

Mdee atoa sharti Chadema kutema ubunge

Spread the love

HALIMA Mdee, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), amesema atatema ubunge wa viti maalum iwapo ‘watakubaliana.’ Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne tarehe 1 Desemba 2020, jijini Dar es Salaam, mwanachama huyo ‘wa hiyari’ wa Chadema amesema, uamuzi wa kutema ubunge utategemea na vikao ndani ya chama.

“Tutakuwa tayari ku – sacrifice (kuutema) ubunge kutokana na vikao vyetu vya ndani,” Mdee ametoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mwandishi kwamba, yupo tayari kuacha ubunge na kurejea kwenye chama?

Akiambatana na wenzake 18 kati ya 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema kutokana na kukiuka misingi ya chama hicho kisha kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu kupitia chama hicho, Mdee amesema uamuzi utakaotokana na vikao vyao vya chama ndio utaonesha hatma yao.

“Jana ndio nilipokea barua ya taarifa ya uamuzi wa Kamati Kuu, kwa maana hiyo mchakato wa rufaa tutaanza kuutafakari kutatua tatizo hili,” amesema.

Amesema, matatizo katika matokeo ya chaguzi kuu yapo miaka mingi akieleza mwaka 2010 na 2015 kulikuwa na sintofahamu, sawa na mwaka 2020 akihoji, kwanini mwaka huu kusiwena wawakilishi bungeni wakati miaka iliyopita walikwenda?

“Chaguzi zote kulikuwa na shida, uchaguzi wa mwaka 2010, 2015 na hata 2020 kulikuwa na sintofahamu, lakini kwanini mwaka huu wasiende bungeni?

“Hivi sasa tunavyoongea madiwani wanaapa, wabunge waliochaguliwa wameapa na msishangae sisi ama wengine wataenda,” amesema Mdee.

Amesema, suala la kutokubaliana kwenye matokeo ya uchaguzi sio sababu ya kuacha kushiriki kwenye vyombo vya maamuzi akisisitiza “… ni ujinga kukimbia vyombo vya maamuzi.”

Amesema, yeye na wenzake wana historia kubwa ya ujenzi wa Chadema na kwamba, bado wapo sana kwenye chama hicho na kwa sasa ni wanachama wa hiyari baada ya kuvuliwa uanachama wiki iliyopita.

“Kwa sasa sisi ni wanachama wa hiyari, ving’ang’anizi, hatuna mpango wa kuondoka Chadema…,tunaipenda Chadema na hatutaondoka Chadema.

“Sisi ni Chadema kindkakindaki, hatuondoki. miongoni mwetu wapo waliokaa Chadema miaka  mitano, 10, 15 na hata 16 kama mimi. Wote tumeijenga Chadema licha ya changamoto tulizopitia, tutabaki Chadema,” amesema.

Mdee alikuwa anazungumza kwa niaba ya wenzake 18 ambao kwa pamoja tarehe 27 Novemba 2020, kamati kuu iliazimia kuwafukuza uanachama wakituhumiwa kwa usaliti wa kujipeleka bungeni kuapishwa bila chama kuwateua.

Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa ni wale waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Ester Bulaya na Esther Matiko. Katibu Mkuu wa Bavicha, Nusrat Hanje. Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Grace Tendega.

Makamu Mwenyekiti Bawacha (Bara), Hawa Mwaifunga. Naibu Katibu Mkuu Bawacha, Jesca Kishoa  na Katibu Mwenezi Bawacha, Agnesta Lambat.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Mtwara, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao.Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza jana jijini Dodoma mara baada ya kumaliza kuwaapisha, Humphrey Polepole na Riziki Lulida kuwa wabunge alisema, Mdee na wenzake ni wabunge halali.

“Wabunge wote walioapishwa ikiwemo wale 20 wa Chadema, 19 na yule mmoja wa jimbo Aida Khenan ni wabunge halali. Niwahakikishe, wale 19 ni wabunge halali, labda wao wenyewe kwa mujibu wa Katiba yetu wapende wajiuzulu,” alisema Spika Ndugai akissitiza, hilo la kufukuzwa kwao yeye halitambui.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!