Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tetemeko ardhi laua Polisi Mwanza
Habari MchanganyikoTangulizi

Tetemeko ardhi laua Polisi Mwanza

Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Spread the love

TETEMEKO la ardhi lililopita mkoani Mwanza na kudumu kwa sekunde 10 limesababisha askari Polisi WP. 114674 Joyce Jackson kupoteza maisha wakati akiwa kazini kwake akiendelea kuchukua maelezo ya watuhumiwa, anaandika Moses Mseti.

Tetemeko hilo lilitokea leo majira ya saa 12:46 hadi 12:56 na kusababisha Polisi huyo kukumbwa na umauti na kuibuka taharuki kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani ambako tetemeko lilikopita.

Inaelezwa kwamba wakati Polisi huyo ambaye alikuwa na wenzake wawili wakiendelea kuchukua maelezo ya watuhumia ghafla walisikia kishindo kikubwa kutoka ardhini na kupata mshituko na kumsababishia kifo.

Pia inaelezwa kuwa wakati anapelekwa hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani hapa ambako alikuwa anafanyia kazi alipoteza maisha huku mwenzake aliyefahamika kwa jina la WP Stella akipoteza fahamu baada ya kusikia mwenzao kafariki dunia.

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (SACP), Ahmed Msangi, aliuambia MwanaHALISI Online, kuwa marehemu Joyce alipoteza maisha wakati akipelekwa hospitalini.

Kamanda Msangi, amesema kuwa askari huyo alipata mshituko mkubwa kutokana na tetemeko hilo lililoibua taharuki kwa wakazi wengi wa mkoa huo huku akidai kwamba alikuwa na tatizo la kupanda kwa presha.

“Pia kuna askari Polisi mwenzake amepata mshitiko baada ya kusikia Joyce (Jackson) amefariki na pia kuna mtuhumiwa mmoja (Mathias Simon) na yeye alipata mshituko kutokana na tetemeko hilo,” amesema Msangi.

Hata hivyo, Kamanda Msangi, amedai kwamba polisi wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini kama kuna watu wengine waliokumbwa na tetemeko hilo ili taarifa zaidi zitolewe kwa umma.

“Hata hapa ofisini kwangu (kituo kikuu cha polisi) tulipata taharuki sana na kuanza kukimbia kutoka ofisini ni kitu cha ghafla ambacho hatukutarajia na tetemeko hili ni la tatu kutokea tangu nifike hapa Mwanza,” amesema Kamanda Msangi.

Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza, akiwemo Meneja wa kampuni ya Bima ya Jubelee, Jared Awando, amesema kuwa wakati tetemeko hilo lilisababisha kukimbia kutoka ofisini kwake.

Awando amesema kuwa tetemeko hilo ambalo limeibua taharuki kwa wakazi wa mwanza, litakuwa limesababisha madhara sehemu nyingine hivyo mamlaka husika inapaswa kuchunguza kiundani suala hilo.

“Labda kuna watu wengine watakuwa wameathirika na tetemeko hili kama lilivyowakumba ndugu zetu wa Kagera na mali kuharibika hivyo mamlaka zinapaswa kuendelea kutoa elimu,” amesema Awando na kuongeza:

“Ninashkuru sijapata tatizo lolote na ninawashauri wananchi wawe watulivu na kama wataalamu wanavyoshauri pindi tetemeko linapotokeo watoke ndani wakae sehemu ambayo ni salama.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

error: Content is protected !!