Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amepata ajali mbaya ya gari akiwa njiani kureje Dar es Salaam akitokea Dodoma, anaandika Hamisi Mguta.
Mkude alikuwa akirejea mjini humo baada ya jana Simba kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho.
Katika gari hilo , lililokuwa na baadhi ya mashabiki wa timu hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Landcuiser kupasuka taili na kuanguka.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Shose Fidelis amefariki dunia katika ajali hiyo.
Mkude ni miongoni mwa majeruhi watatu ambapo wawili wamewahishwa katika hospitali ya Morogoro walioambatana na Shose na wenzake kwenda kuishangilia Simba ikipambana kuwania Kombe la Shirikisho.
Shose amekuwa miongoni mwa mashabiki wakubwa wa Simba na amekuwa akionekana pamoja katika lile Kundi la Wapenda Soka ambalo linaundwa na mashabiki wa Simba.

Leave a comment