Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mwijage ajifananisha na Gaddafi
Habari za SiasaTangulizi

Mwijage ajifananisha na Gaddafi

Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Picha ndogo Marehemu Muhammed Gaddafi
Spread the love

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema yeye ni muumini wa Mohammed Gaddafi, kwa kueleza kuwa yeye anafanya kazi ya kujenga mbali bila kujenga kwao na atajenga kwao mwishoni, anaandika Dany Tibason.

Licha ya Mwijage kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji pia ni mbunge wa Muleba Kaskazini, amesema yeye hawezi kujenga kwao kwanza na badala yake anaaza kujenga mbali na kwake kwa maana ya nyumbani kwake atajenga mwishoni wakati kaisha maliza sehemu nyingine.

Alitoa kauli hiyo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Sevelina Mwijage (CUF).

Sevelina katika swali lake la nyongeza alitaka kujua ni kwanini Waziri huyo ambaye anatokea katika mkoa wa Kagera ambaye ni mzawa wa Kagera na anaijua vizuri Kagera asianzishe kiwanda cha kuchakata mazao ya kahawa na chai ambalo ni zao linalolimwa mkoani humo.

“Waziri wewe ni mzaliwa wa mkoa wa Kagera ni kwanini usifikilie kuanzishwa kwa viwanda vya kuchakata zao la kahawa na majani ya chai ili wananchi kuondokana na umasikini,” amehoji Sevelina.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Ileje, Janet Mbene (CCM) alitaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuanzisha viwanda vidogo ili kuongeza ajira kwa wananchi na kukupa pato la serikali.

Akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Mwijage amesema kuwa yeye ni Muumini wa Muhammad Gaddafi kwani hawezi kujenga nyumbani kwanza anaanza na mbali anamalizia na nyumbani.

Pia amesema kwa sasa ameanzisha mazungumzo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata maziwa ambacho kinaweza kufanya kazi vizuri.

Akijibu swali la msingi Mwijage amesema ili kutekeleza mikakati ya ujenzi wa viwanda, mamlaka za mikoa na wilaya zimeelekezwa kutenga maeneo mahususi kwa ajili ya kujenga viwanda vidogo vya kati na vikubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!