Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu
Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Charles Kichere
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicheere ametoa hati mbaya kwa Wakala wa Umeme na Ufundi Tanzania (TEMESA) ikiwa ni miezi kadhaa tangu kuibuka kwa sintofahamu kuhusu gharama ya ukarabati wa kivuko cha MV-Magogoni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

TEMESA ni miongoni mwa taasisi tatu zilizopata hati mbaya kati ya hati 1,045 zilizotolewa na CAG katika ukaguzi wa hesabu wa mwaka 2021/2022.

Hivi karibuni mjadala wa gharama za ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni kwa Sh 7.5 bilioni wakati chenyewe kilinunuliwa kwa Sh 8.5 bilioni uligonga vichwa vya habari na kuibua maswali mengi juu ya uhalali wa kiwango hicho cha fedha.

Katika mjadala huo mambo yaliyoibuka ni pamoja na zabuni ya ukarabati huo kutolewa kwa kampuni ya kigeni badala ya kampuni za ndani, huku wengine wakihoji kuwa fedha zote hazikuwa kwenye bajeti ya mwaka huu.

Katika ufafanuzi wake TEMESA ilisema mzabuni aliyepewa kazi hiyo ndiye alikuwa na gharama ya chini kuliko hata wale wa ndani walioomba. Ilieleza pia kuwa tofauti ndogo ya gharama ya ukarabati n aile ya kununulia kivuko hicho inatokana na tofauti ya kubwa ya gharama za vipuri kipindi kinanunuliwa na sasa.

Kivuko cha Mv Magogoni kilichoanza kazi mwaka 2008 kikiwa na uwezo wa kubeba tani 500 (sawa na abiria 2,000 na magari madogo 60), ni kiunganishi muhimu kati ya Kigamboni na Magogoni.

Taasisi zingine zilizopata hati mbaya mbali na TEMESA ni Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu na chama cha siasa cha Sauti ya Umma (SAU).

Akisoma taarifa ya Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Mwaka 2021/22 mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jiji Dar es Salaam leo, Kicheere amebainisha kuwa taasisi 1,010 zimepata hati zinazoridhisha sawa na asilimia 96.64, taasisi 29 zimepata hati hati zenye shaka sawa na asilimia 2.8.

Amesema hati chafu ni tatu sawa na asilimia 0.29 na hati alizoshindwa kutoa maoni ni tatu sawa na asilimia 0.29.

2 Comments

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI..

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA… MHE. KULE ULIKOOA KUNA JAMBO LETU LA KATIBA MPYA… ULIKOOA ULIPELEKA NYOTA YA WATU KUSHINDA BIKO KILA SIKU

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!