Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo
Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema amebaini upotevu wa kodi ya zuio ya Sh 749 uliotokana na kutokukusanywa na kuwasilishwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ … (endelea).

Miongozi mwa taasisi sita zilizotajwa kukusanya kodi hiyo na kutoiwasilisha TRA ni Chama cha ACT-Wazalendo ambacho kilizuia Sh 8.5 milioni lakini haikuwasilisha TRA.

Kicheere amebainisha hayo leo Jumatano tarehe 29 Machi 2023 Ikulu ya Dar es salam akimkabidhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Ripoti ya Taarifa za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022.

Amesema taasisi 6 zilizuia kodi lakini hazikuwasilisha TRA Sh milioni 35 kinyume cha sheria.
Alisema taasisi 15 hazikukata kodi ya zuio ya Tsh 713.70 Milioni na taasisi 6 zilizuia kodi na hazikuwasilisha TRA Sh 35 milioni.

Mbali na ACT-Wazalendo taasisi zingine Wizara ya Viwanda na Biashara Sh. 16 milioni.

Taasisi ambazo hazikukusanya kodi ya zuio ni Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Sh 442 milioni, Kampuni ya Ujenzi ya JKT Sh 162 milioni, Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) Sh. 56 milioni na Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (TANEPS) Sh 34 Milioni.

Mbali na hilo Kicheere ameeleza kuwa wamebaini ukusanyaji wa mapato nje ya mfumo wa GePG ambapo RUWASA ilikusanya Sh 68 bilioni, Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasilino Sh 151 bilioni na Shirika la Magereza Sh 900.96 milioni.

“Zote zimekusanywa nje ya GePG na ni kukiuka maelekezo ya Serikali inayoelekeza fedha zote zikusanywe kwa mfumo huo,” amesema Kicheere.

Pia upotevu mwingine wa mapato ni kutokukusanywa kwa ada ya usafirishaji wa mizigo iliyozidi uzito iliyoidhinishwa na Wizara ya Ujenzi na kupoteza mapato ya Sh 41.48 bilioni.

Aidha TBA kutokukusanya kwa kodi za nyumba zilizopangishwa kwa taasisi za Serikali kwa muda wa miezi 10 na kuendelea na hivyo kupoteza mapato ya Sh 13 bilioni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!