Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko TEF kunoa waandishi wa habari kupinga ndoa za utotoni
Habari Mchanganyiko

TEF kunoa waandishi wa habari kupinga ndoa za utotoni

Spread the love

JUKWAA la Wahariri nchini(TEF) limetangaza kampeni ya kutoa elimu kwa waandishi wa habari ya namna ya kuhamasisha jamii kutoa maoni yao kupinga ndoa za utotoni. Anaripoti Marry Victor…(endelea).

Akizungumza katika hafla ya kutoa tuzo kwa waandishi wa habari za watoto, pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alisema kampeni ya kupinga ndoa za utotoni wataishiriki kikamilifu kupinga ndoa za utotoni kwa ajili ya kuhakikisha watoto wanatimiza ndoto na malengo yao.

 

Pamoja na kulishukuru Shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF), Balile alisema kabla ya mradi huo wa habari za watoto kuanza kuendeshwa nchini, msamiati wa udumavu haukuwa ukifahamika katika nchini.

Alisema; ‘Tunawashukuru Wahariri kwa kuwafahamisha wananchi mambo kama haya. Lakini tunawashukuru waandishi wa habari kwa kutumia gharama, muda wetu katika kuitafuta habari hizi za watoto, gharama mnazozitumia ni kubwa kuliko kiwango cha zawadi mnazotunukiwa leo.

“Niwaombe UNICEF ushirikiano huu uliozaa matunda msituache. Kipekee namshukuru Neville Meena kwa kusimamia mradi huu bila kukata tamaa,” alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo Guru la uandishi wa habari Salim Said Salim alisema lengo la hafla hiyo ya kutoa tuzo ni kuhamasisha maendeleo katika kuandika habari za watoto.

“Ushindani huu tulioukusudia katika uandishi wa habari ni kushawishi waandishi wa habari kuleta mabadiliko katika jamii kuhusu malezi ya watoto. Ombi langu kwa wanajamii ni moja kama tunazaa basi tuwalee watoto, tuwahudumie, tuwatunze na tuwalinde,” alisema.

Naye Jesse Kwayu Mjumbe Kamati ya Mradi wa habari za watoto alisema kazi hiyo ya kuwa na habari za watoto ni kuwapa watoto kipaumbele waweze kusikika; “Kumekuwa na kazi nzuri zimefanyka habari 76 zimeandikwa na kutangazwa.

“Ni mafanikio makubwa pamoja na mafanikio haya yako mambo ya kuangalia tangu 2017 na leo tunaingia 2023 kuna impact gani,” alisema.

Jesse aliongeza kwa kuweka msisitizo katika kuhamasisha umma kutoa maoni yao kupinga sheria inayoruhusu ndoa za utotoni.

Alisema;”Kutoka hapa tunafanya nini katika sheria ya ndoa . Je waandishi kwa ujumla wetu tunaifahamu  hii sheria ya ndoa ya 1971?

“Lengo tujikiite kufanya kampeni ili iweze kufanyiwa mabadiliko lengo mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 aweze kutimiza malengo na si kuolewa katika umri mdogo ambao ni chini ya miaka 18,” alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo waandishi mbalimbali walipata tuzo za uandishi wa habari bora za watoto, Naibu Muwakilishi wa UNICEF nchini, Ousmane Niana pamoja na mambo mengine alipongeza TEF kwa kufanikisha hafla hiyo pamoja na kupongeza mapambano ya kuandika habari za watoto na kupunguza hali ya utapiamlo nchini.

“Tanzania inatakiwa kuendelea kuhamasisha kuzuia watoto kuolewa wakiwa na umri mdogo ili wasome na kufikia ndoto zao.

“Pia iendeleze mapambano dhidi ya maambukizi Covid 19 kupitia vipindi vya redio pamoja na habari kupinga mimba za utotoni pamoja na watoto kwa ujumla,” alisema.

Miongoni mwa waliotunukiwa katika hafla hiyo ni pamoja Aidan Mhando (Channel Ten) kutoka mkoani Simiyu, Faraja Masinde (Mtanzania digital) kutoka jijini Dar es salaam, Arnod Kalembo kutoka mkoani Kagera, Stansilaus Lambart na wengine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!