RIPOTI ya Usalama kuhusu maendeleo ya Jeshi la Watu wa Jamhuri wa China iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani ninaonyesha kuwa jeshi hilo limeongeza uzalishaji wa vichwa vya nyuklia ambapo inakadiriwa kufika silaha 1,000 mwaka 2030. Imeripotiwa na ukurasa utafiti na masuala ya kiusalama katika bara la Asia ORCA … (endelea).
Waachambuzi wa masuala ya usalama wanaitaja hali hiyo kuwa inaweza kuwa tishio kwa jirani zao taifa la India kutokana na utamaduni wa uchina kufanya uchokozi kwenye mipaka ya nchi hizo mbili.
India inapakana na China kwa upande wake wa Kaskazini jambo ambalo litajwa kuwa linaweza kuzua hofu au kutoa changamoto ya uimarishaji vikosi vyake.
Wanaduru wanaeleza kuwa China imejikita kwenye utengenezaji wa silaha hizo ili kujihami dhidi ya Marekani pia kujenga uwezo wake wa kujilinda.
Lakini mtazamo wa hofu kwenye mpaka wa India upo palepale kwa kuwa China haitokoma kufanya uchokozi mipakani.
Wachambuzi wa masuala ya usalama duniani wameipa hadhari India kwa kuishauri kujiweka imara kijeshi kujimarisha hata ikitamani kulipa kisasi basi itakuwa imara zaidi.
Leave a comment