
Mhandisi Andrew Kisaka, Mkuu wa Idara ya Leseni TCRA
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesitisha kutoa leseni mpya za maudhui ya mtandaoni (Online TV na Blogs). Anaripoti Yusuph Katimba, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Ijumaa tarehe 5 Februari 2021, Mhandisi Andrew Kisaka ambaye ni Mkuu wa Idara ya Leseni TCRA, amesema maombi mapya ya leseni yamesitishwa kuanzia sasa.
“Leseni mpya kwa ajili ya maudhui ya mtandaoni zimesitishwa mpaka tarehe 30 Juni 2021,” amesema Kisaka.
Amefafanua, kwamba wateja wenye leseni ambao wanataka kuhuisha, wanaruhusiwa kuendelea kufanya hivyo wakati wowote.
“Kwa wale ambao wanazo leseni na wanataka kuzihuisha, hawa wanaruhusiwa. Kilichositishwa ni utoaji wa leseni mpya mpaka tarehe hiyo,” amesema.
Hata alipoulizwa sababu za mamlaka hiyo kuamua kusitisha utoaji wa leseni mpya, Kisaka amesema “tunataka kufanya tathmini ya maudhui ya mtandaoni kwa sasa.”
More Stories
Milioni 30 kuhifadhi misitu ya vijiji Morogoro
Bosi Tarura aagiza ujenzi daraja Kaseke, 1.5 milioni zirejeshwe
Operesheni Samia yawapatia vijana 45,047 mafunzo JKT