Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ndugai ashtushwa gharama mashine za upumuaji
AfyaHabari za Siasa

Ndugai ashtushwa gharama mashine za upumuaji

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameshtushwa na gharama kubwa za mashine za kusaidia upumuaji kwa watu wenye tatizo hilo, zinazotolewa katika hospitali binafsi nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma jana, Alhamisi tarehe 4 Februari 2020, Spika Ndugai ameitaka wizara ya afya ifuatilie suala hilo, kuhakikisha gharama hizo zinapunguzwa mara moja.

Spika Ndugai alieleza kuna taarifa zisizothibitishwa, baadhi ya hospitali binafsi zinatoza Sh.1 milioni kwa siku, wagonjwa wenye matatizo ya kupumua wanaotumia mashine za kupumua (Ventilator).

“Nimeona Naibu Waziri wa Afya (Dk. Godwin Mollel) yuko hapa, naambiwa sina hakika wakati huu kuna baadhi ya hospitali za private (binafsi) hasa Dar es Salaam mashine za kupumua kuna baadhi zinachaji Sh.1 milioni, 850,000 au 700,000 kwa siku,” alisema Spika Ndugai.

Spika Ndugai alisema “nikasema yarab toba, hata kama za private iko haja ya wizara kuangalia hilo jambo. Ndio maana nasema ni bora 200,000 kwa wakati mmoja, sasa hii Sh.1 milioni kutwa, mwaka ni Sh.365 milioni endapo jambo hilo ni kweli.”

Spika Ndugai alitoa ombi hilo katika mjadala wa wabunge kuhusu Hotuba ya Rais John Magufuli ya kufungua shughuli za Bunge la 12, aliyoitoa tarehe 13 Novemba 2020.

Baada ya Mbunge Viti Maalumu, Kunti Majala kulalamika gharama kubwa za vipimo vya CT Scan, akisema, Watanzania wengi hawawezi kumudu bei ya Sh. 200,000.

Spika Job Ndugai

Akichangia hoja hiyo, Spika Ndugai alisema bora ya gharama za vipimo vya CT Scan wananchi wanaweza kumudu Kuliko gharama za matibabu ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua ambao baadhi yao hutozwa hadi Sh. 1 Mil kwa siku.

“Kunti umeongelea habari ya CT Scan Sh. 200,000, lakini ile ni mara moja ukipimwa unaendelea na mambo mengine hurudi kesho na kutwa,” alisema Spika Ndugai.

Wito huo wa Spika Ndugai umekuja siku moja tangu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Mabula Mchembe kutaka hospitali binafsi kutopandisha bei za matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya kupumua.

Prof. Mchembe alitoa katazo hilo alipotembelea Hospitali za Agakgan na Kairuki zilizoko jijini Dar es Salaam, kwa akikagua hali ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.

1 Comment

  • Hospitali ya Aga Khan kitanda cha kulala tu ni milioni sembuse mashine na matibabu
    Wakati mmoja Rais Magufuli alimueleza Bwana Aga Khan mwenyewe kuhusu gharama hizi za ajabu naye AK akasema ataliangalia. Mpaka leo hakuna kilichofanyika. Serikali iliangalie hili
    Kulazwa tu hapo unatakiwa uweke milioni sita. Matokeo yake wengi wa wagonjwa hapo ni wale wenye bima za kigeni. Bima ya taifa NHIF hawaikubali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

error: Content is protected !!