Sunday , 3 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Tatizo la moyo lapiga kambi kanda ya ziwa
Habari Mchanganyiko

Tatizo la moyo lapiga kambi kanda ya ziwa

Wataalamu wa Upasuaji wa Moyo wakiendelea na kazi
Spread the love

ASILIMIA 15 ya wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza, kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa kupima afya zao wamebainika kuwa na tatizo la ugonjwa wa moyo,  anaandika Moses Mseti.

Hospitali hiyo ya rufaa inayowahudumia wagonjwa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, imejidhatiti kuhakikisha inatoa huduma ya magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo na Vifua Professa. William Mahalu wakati wa upimaji bure wa ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu, lililoendeshwa na hospitali hiyo katika kuelekea kilele cha siku ya moyo duniani, Septemba 30 mwaka huu.

Professa Mahalu amesema kuwa tatizo la moyo na shinikizo la damu nchini limeonekana kuwakumba watu wengi na kwamba kwa miaka ya hivi karibuni limeonfezeka kutokana na watu wengi kushindwa kupima afya zao mara kwa mara ili kuchukua hatua mapema.

Amesema ugonjwa wa moyo ni hatari kwa binadamu na kwamba watu wengi wamekuwa wakitembea na kuishi na ugonjwa huo bila kufahamu.

“Miaka mitano ijayo hatutarajii kupeleka wagonjwa Muhimbili (Hospitali ya Taifa) wala Taasisi ya Jakaya Kikwete, tutakuwa tunaitoa hapa (Bugando) kwa kuwa siku za nyuma baadhi ya vifaa na watalaamu walikuwa hawapo,” amesema.

“Tunaamua kutoa huduma hii bure kutokana na watu wengi kushindwa kumudu gharama za matibabu ya ugonjwa wa moyo kwa kuwa gharama ya oparesheni ya moyo ni  shilingi milioni sita kiasi ambacho ni kikubwa ,” amesema Professa Mahalu.

Professa Mahalu ametaja sababu zinazochangia kuongezeka kwa ugonjwa huo wa moyo kuwa ni uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe,  kula chakula chenye mafuta mengi,  kula chumvi ndani ya chakula na watu wengi kushindwa kufanya mazoezi.

Mkurugenzi wa Huduma na Tiba wa Bugando, Dk. Merchedes Bugimbi, amesema wameamua kuendesha na kutoa huduma hiyo bure kwa wananchi baada ya wagonjwa walio wengi kushindwa kumudu gharama za matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Dk. Bugimbi amewahakikishia wananchi wa mikoa ya kanda hiyo kwamba hospitali ya hiyo hivi sasa ina vifaa na madaktari bingwa wa kutosha na kwamba oparesheni za moyo zitakuwa zinatolewa hospitalini hapo bure.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Habari Mchanganyiko

TARURA kujenga madaraja 189 kwa teknolojia ya mawe

Spread the loveWakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imejipanga kujenga...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

error: Content is protected !!