February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi  wavuruga UVCCM Mwanza 

Umoja wa Vijana CCM (UVCCM)

Spread the love

UCHAGUZI wa marudio wa kumtafuta mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM), katika wilaya ya Nyamagana jijini Dar es Salaam zimegubikwa vurugu, anaandika Hamis Mguta.

Vurugu hizo vimeibuka baada ya wajumbe kutoka Kata ya Mahina kuzuiwa kuingia ukumbini kupiga kura kwa madai ya kuwa si wajumbe halali.

Katibu wa wajumbe hao, Samora Msiba amesema baada ya kuhoji sababu ya wao kuzuiwa kuingia ukumbini walielezwa kiongozi wao wa kata hana mawasiliano au mahusiano mazuri na serikali.

“Tunaomba viongozi wa ngazi za juu waliangalie suala hili kwa kuwa hata sisi tuna haki ya kupiga kura na si kusukumwa na kususiwa ovyo kwa kuhusishwa na kesi zisizotuhusu,” amesema Msiba.

Hata hivyo, chanzo chetu kinaeleza kuwa vurugu zimesababisha walinzi wa chama hicho (Green Guard) kuzuiwa kufanya kazi yao na badala yake mgambo wa Jiji la Mwanza kusimamia uchaguzi huo.

Kuhusu kuzuiliwa kwa walinzi hao wa Green Guard, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mahina ambaye pia ni Katibu wa Green Guard wilayani humo Kagambo Paul amesema amekerwa na kitendo cha kuporwa jukumu lake la kusimamia uchaguzi na kupewa jeshi la akiba la mgambo.

Uchaguzi kwa mara ya kwanza ulifanyika Septemba 23 ambao mshindi hakupatikana kutokana na kura kutofikia nusu ya zilizopigwa.

error: Content is protected !!