Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania, Zambia zakubaliana kujenga TAZARA kwa kiwango cha SGR
Habari za Siasa

Tanzania, Zambia zakubaliana kujenga TAZARA kwa kiwango cha SGR

Spread the love

 

TANZANIA na Zambia zimekubaliana kuanzisha mradi wa pamoja wa kuboresha reli ya TAZARA kwa kiwango cha kisasa (SGR). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Marais wa nchi hizo mbili Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Hakainde Hichilema wa Zambia wamekubaliana wamekubaliana kutafuta fedha kwa pamoja na kujenga reli hiyo kwa kiwango cha SGR.

Rais Chikwende yupo Tanzania kuanzia leo Jumanne tarehe 2 Agosti, 2022, kwa ziara ya kiserikali ambapo alipokewa na mwenyeji wake Suluhu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo alipigia mizinga 21 na kukagua gwaride.

Wawili hao walipata wasaa wakufanya mazungumzo na baadae kuzungumza na vyombo vya habari katika Ikulu ya Dar es Salaam ambapo walieleza kile walichozungumza na kukubaliana.

“Tumekubaliana tuboreshe TAZARA kama tunaifanyia marekebisho reli iliyopo lakini tukakubaliana kwamba kwa dunia ya leo reli ni SGR, kwahiyo tukakubaliana kuwa na mradi wa pamoja tutafute pesa kwa pamoja kupitia PPP pengine na marafiki waliotujengea hiyo reli tuone jinsi tutakavyoboresha kwa kiwango cha SGR,” amesema Rais Samia.

Reli ya TAZARA ilijengwa kwa kiwango cha Meter Gauge (MG) kwa ushirikiano wa nchi mbili za Tanzania na Zambia ikiunganisha majiji ya kibiashara mawili ya nchi hizo Dar es Salaam upande wa Tanzania na Ndolwa upande wa Zambia.

Mbali na TAZARA, amesema hata bomba la kusafirisha mafuta ghafi la TAZAMA halifanyi kazi kama ilivyokusudiwa kutokana na kuwa ni dogo na mabadilko ya sera za nishati za Zambia.

“Zambia wamebadilisha sera zao kwenye mambo ya energy (nishati) na sasa wanakwenda kuagiza bidhaa za petroli ambazo zimetimia badala ya mafuta ghafi.

“Tumekubaliana bomba lile (TAZAMA) ni dogo sana kwahiyo kuna haja ya kujenga kubwa litakalopeleka mafuta kwa wingi na bandari ya Dar es Salaam na facilities (miundombinu) zilizopo Tanzania ziwasaidie kupunguza ughali wa mafuta katika nchi yao,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!