August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani yamuua kiongozi wa Al-qaeda kwa ndege zisizo na rubani

Aymam Al-zawahiri

Spread the love

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden, amesema kiongozi wa Al-qaeda, Aymam Al-zawahiri, ameuawa katika shambulio lililofanywa na Marekani nchini Afghanistan. Anaripoti Erick Mbawala kwa msaada ya mitanadao ya kimataifa … (endelea)

Biden, amethibitisha shabulio la mauaji hayo usiku wa Jumatatu hii tarehe 1 August ambapo amesema kuwa kiongozi wa Al-qaeda Aymam Al-zawahiri, ameuawa kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani ambazo zimefanywa na jeshi lake.

“Amekuwa akiongoza makundi ya kigaidi na kufanya mauaji kwa wananchi, wanadiplomasia na wahudumu wa kimarekani,” amesema Biden akiwa Ikulu ya White House.

Marekani imefanya shambulio lake la kwanza nchini Afghanistan kwa kutumia ndege zisizo na rubani tangu kuondoka kwa wanajeshi wake Agosti 2021.

Joe Biden, Rais wa Marekani

Al-zawahiri, alichukua cheo hicho baada ya aliyekuwa kiongozi wa kikundi hicho Osama Bin Laden , kuuawa na vikosi vya Marekani mwaka 2011, na ameripotiwa kuwa na matukio kadhaa ya kigaidi nchini Marekani barani Afrika na kusababisha mauaji ya watu wengi.

Al-zawahiri pia amewahi kutumikia kifungo baada ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa Rais wa Misri mwaka 1981 kabla hajawa kiongozi wa Al-qaeda.

Inaelezwa kuwa vikosi vya Kimarekani vilimnasa kiongozi huyo ambaye alikuwa amejificha Afghanistan mjini Kabul kabla ya makombora mawili ambayo yalirushwa kwa kutumia ndege zisizo na rubani Jumamosi hii, July 30 2022.

error: Content is protected !!