SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco), limetangaza bei mpya ya kuunganisha umeme mijini na vijijini kuanzia leo Jumatano tarehe 5 Januari 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Bei hizo zimetangazwa ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipomwagiza Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwenda kusimamia suala hilo.
Alisema bei ya Sh.27,000 iliyokuwepo awali, haiendani na uhalisia hivyo kusababisha Tanesco kushindwa kutekeleza miradi ya kusambaza umeme kwa wakati.
Katika kutekeleza hilo, Tanesco imetoa bei mpya zinazojumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) huku kwa wateja wa vijijini wa njia moja ikibaki ile ile Sh.27,000.

Kwa wateja watakaohitaji kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme itakuwa Sh.320,960, kwa mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme Sh.515,618, umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme Sh.696,670.
Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme Sh.912,014, kwa mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme Sh.1,249,385, umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme Sh.1,639,156.
Leave a comment