Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aagiza bei ya kuungiwa umeme ipande, Waziri Makamba asema…
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia aagiza bei ya kuungiwa umeme ipande, Waziri Makamba asema…

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kufutwa kwa kiasi cha awali cha Sh.27,000, kilichokuwa kinatozwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwaunganishia umeme watejwa wapya kwa maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …  (endelea).

Gharama ya kuunganishiwa umeme wa njia moja ilipungua hadi Sh.27,000 kutoka Sh.177,000 katika maeneo ya vijijini au mijini wakati wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Jana Jumanne tarehe 4 Januari, 2022, akizungumza Ikulu ya jijini Dar es Salaam, Rais Samia alikiri kwamba Tanesco na Waziri wa Nishati, Januari Makamba walikuwa ‘wamezibwa mdomo’ kuhusu uhalali wa kiasi kilichokuwa kinatozwa.

“Najua waziri (January Makamba) amekuwa kimya, lakini nimekusaidia kusema. Tanesco inapoelekezwa kutoza Sh.27,000 tu kwa kila kitu kipya, swali kuu huwa, je, inapata wapi fedha za ziada,” aliuliza.

Aliagiza kuanzia sasa wateja wapya wanaohitaji kuunganishiwa umeme watatozwa ada mpya lakini kwa watu wanaoishi vijijini ndio watakaofaidika na sera ya tozo hiyo ya Sh 27,000.

MwanaHALISI Online, limezungumza na Waziri Makamba leo Jumatano kuhusu utekelezaji wa agizo hilo amesema, wanalifanyia kazi, “na leo tutatoa taarifa” kwani Rais amekwisha agiza, sisi wasaidizi wake ni kutekeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!