October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yamhoji Sethi

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 8 Novemba 2018 imeelezwa kwamba mtuhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi amechukuliwa maelezo yake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wakili wa Takukuru, Leornad Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ameieleza mahakama hiyo kuwa, jana walifanikiwa kuchukua maelezo ya Sethi.

Wakili Swai ameieleza mahakama kuwa, baada ya Takukuru kuchukua maelezo ya Sethi, wanaendelea na hatua za upelelezi zinazofuata.

Kufuatia kauli hiyo, Wakili wa Sethi, David Chillo aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo.

Hakimu Shaidi kutokana na maelezo ya pande zote mbili, aliiahirisha kesi hiyo hadi tarehe 22 Novemba 2018, siku ambayo tarehe itakapotajwa, pamoja na kuangalia kama upelelezi umekamilika au bado.

error: Content is protected !!