Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Hii ni Jahannam katika uso wa dunia
Makala & Uchambuzi

Hii ni Jahannam katika uso wa dunia

Spread the love
UNAWEZA kujiuliza, kwanini wanadamu wamekuwa na tabia za ovyo zaidi ya wanayama wakali? Nini hasa walichojisahau mpaka kutojali maumivu wanayopata wengine? Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).
Dunia inabagua, inajielekeza kule kwenye maslahi yao binafsi. Mataifa yanayoonekana kutokuwa na maslahi na wakubwa, yanapigwa teke. Yanateketea.
Kuuawa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Washington DC raia wa Saudi Arabia na namna mataifa makubwa yalivyolisimamia, unaweza kudhani ndio mauaji mabaya zaidi kutokea kwa sasa.
Lakini unapotupia jicho Yemen, unistaajabu dunia na waliopewa mamlaka katika kusimamia vilivyomo. Khashoggi hakustahili kuuawa kama ambavyo raia wa Yemen wanavyostahili kufurahia maisha.
Taswira ya taifa la Yemen leo inamuumiza kila aliye na moyo wa ubinaadamu. Hii haijalishi dini, kabila ama utaifa. Yemen ipo katikati ya dimbwi la damu huku dunia ikijitoa lawamani.
Njaa, mateso na hekaheka za kila siku zimekuwa sehemu kuu ya maisha ya raia wa Yemen. Imetengwa na sasa ni kama mtoto yatima.
Katika ardhi ya Yemen maelfu ya watoto wanaaga dunia kila mwaka kutokana na utapiamlo na magonjwa yanayoweza kuzuilika.
“Yemen leo hii imegeuka na kuwa jahanamu ambayo si kwa ajili ya asilimia 50 hadi 60 ya watoto tu ya watoto wa nchi hiyo, bali ni jahanamu kwa kila mvulana na binti wa Yemen.” Anasema Mkurugenzi wa Kanda wa Maeneo ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika wa Unicef-Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa.
Wakati maisha katika mataifa mengine yaliendelea, Taifa la Yemen linazidi kuzama kwenye. Waasi wa Houthi ndio wanaoiendesha puta nchi hiyo.
Kinachofanywa na Saudi Arabia ni kutoa msaada wa karibu kwa wapiganaji wa serikali ambao nao ni dhoofu.
Jumuiya za kimataifa hazilipi uzito unaostahili suala la machafuko nchini Yemen, Saudia inajitosa kwa kuwa nao ni waathirika wa moja kwa moja na machafuko hayo.
Maisha yanahuzunisha, watoto na wanawake wanauawa, wanaobaki hai wanaishi kwenye tishio kubwa la njaa, kukosa maji na huduma uhimu za kibinaadamu.
Yemen inakumbwa na mtikisiko kama ilivyo Syria, Iraq na mataifa mengine ya kiarabu, lakini msaada na kuliseme taifa hilo kupo kwa kiwango cha chini zaidi.
Taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa, waasi wa Houthi wanapata nguvu kutoka katika Serikali ya Iran. Ni kwa kuwa, Serikali ya Yemen ina mrengo tofauti na serikali ya Iran.
Lakini hapo hapo Serikali ya Yemen ina ukaribu zaidi na Serikali ya Saudia, wakati Saudia ina uadui mkubwa na Serikali ya Iran.
Mara kadhaa Sausia imekuwa ikilalamikia makombora yanayoelekezwa Riyadh kutoka kwa waasi wa Houthi ambao ndio maswahiba wa Serikali ya Iran.
Mkanganyiko huu kwa kiwango kikubwa umesababisha kupungua kwa juhudi za kutafuta suluhi kwa kuwa, malengo ya mataifa jirani na Yemen yanatofautiana katika mgogoro unaoendelea nchini humo.
Taarifa mbalimbali za kichunguzi zinaeleza kuwa, Yemen imeacha na jumuiya za kimataifa katika mapambano yake dhidi ya Houthi.
Hatua hiyo imesababisha waasi hao kuwa na nguvu kubwa na kukalia maeneo mbalimbali ya ardhi ya Yemen kwa mabavu.
Hata hivyo, pamoja na juhudi ndogo zinazoonesha na mataifa ya nje, njia kadhaa zimeshauriwa kuhakikisha taifa hilo linaondoka kwenye mgogoro unaoumiza wengi.
Tayari waasi wa Houthi wamejitengenezea himaya yao ambapo wanakusanya kodi na kusambaza huduma huku wananchi wakilipa kwao.
Hatua ya kuwa ‘serikali’ na mkusanya kdi mkuu inaongeza uimara wa Houthi huku serikali ya Yemen ikiendeleza kutafuta mbinu za kuangamiza kundi hilo.
Mfano, Bandari ya Hodeidah inashikiliwa na waasi wa Houthi na kufanya sehemu muhimu ya kuingiza silaha na huduma mbalimbali ndani ya taifa hilo.
Wakazi wanaoizunguka Hodeidah kwa sasa hawajui nini kianednelea. Wanachoamini ni kuwa, wapo kwenye hatari na uokozi kwao ni kama ndoto.
Maisha ya wakazi hao yamejawa na sintofahamu, huduma za kijamii kama maji, chakula na matibabu yanahitajika kwa kiwango kikubwa lakini mazingira ni magumu.
Inaaminika kuwa, ukombozi wa Hodeidah unaweza kufungua huduma muhimu kwa nchi zote kwa kuwa, ni mdomo wa huduma kwa taifa hilo.
Ni eneo muhimu linalotumika kupitishia huduma za kijamii. Waasi wa Houthi wameshikilia bandari hiyo kwa muda mrefu sasa.
Wanatumia bandari hiyo kusafirishia silaha, wanajeshi na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika vita yao dhidi ya Serikali ya Yemen.
Lakini bandari hiyo imekuwa kitovu cha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ikiwemo hospitali, makazi ya wananchi pia makombora wanayoelekeza nchini Saudi Arabia.
Waasi hao wamekuwa wakijitanua nakuendelea kuchumua maeneo yaliyokuwa chini ya serikali huku wakiendelea makombora Saudia.
Hivi karibuni waasi hao walielekeza makombora yao Saudia katika mji wa Khamis Mushayt huku tuhuma kubwa zikielekezwa katika Serikali ya Iran kwamba ndio wafadhili wakuu.
Houthis wamekuwa wakitumia Hodeidah kama njia ya kuu ya kujizatiti katika uchumi wa kundi lao. Ni kwa kukusanya kodi, kusimamia biashara pamoja na huduma za kibinaadamu.
Kundi hilo la waasi limekuwa likivuna zaidi ya Dola za marekani milioni 30 kwa mwezi kwa kulitawala eneo hilo na biashara zake.
Kwa kiwango kikubwa, kutawala eneo hilo kumewawezesha kusimamia uingizwaji wa silaha na dawa ambazo wao ndio wanakuwa wafanyabiashara wakuu kwa wananchi wa maneneo hao.
Serikli ya Yemen imeishiwa nguvu hasa baada ya eneo hilo kuwa chini ya waasi, kutokana na mazingira ya kutawala nabdari ya Hodeidah, inavyoelekea ni kuwa serikali haina namna ya kuwapokonya eneo hilo.
Tatizo kubwa linaloitawala Yemen ni kutokana na yenyewe kugawika, hakuna umoja jambo ambalo limekuwa likiwapa nguvu waasi wa Houthis.
Katika ukweli ulio wazi, machafuko ya Yemen yanagharimu kwa kiwango kikubwa mataifa yanayozunguka taifa hilo.
Taifa kama Saudi Arabia na yale yalio kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi jumuiya yapo hatarini.
Pamoja na kwamba waasi kupata msaada kutokana na msaada wa karibu kutoka utawala wa Iran, lakini pia wamekuwa wakipata misaada kutoka kwenye mataifa mengine ambayo bila shaka jumuiya za kimataifa wayajua.
Serikali ya Yemeni pamoja na washirika wake wanapasa kupata msaada wa moja kwa moja kutoka jumuiya za kimataifa kama ilivyoelezwa Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa.
Waasi wa Houthis wamekuwa wakitumia chakula na msaada wa madawa kama ngao ya kuwafanya wananchi kuwakubali hivyo kuelndelea na mikakati yao ya kisiasa kwenye ardhi ya Yemen bila vikwazo kutoka kwa wapinzani wake.
Taifa la Yemene linateketea kutokana na kuzama kwenye njaa ambayo pia inatumiwa na waasi hao kuwageuza wananchi hao ili kuwaona kuwa ni bora zaidi ya serikali yao.
Kuingia kwa Saudia katika kuhakikisha wananchi wa Yemen wanapata huduma kutasaidia kufikisha vyakula na dawa kwa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMakala & Uchambuzi

Kanda ya Ziwa yaonyesha NMB inavyosaidia afya ya mama na mtoto

Spread the loveMafanikio inayozidi kupata Tanzania katika kupunguza vifo vya mama na...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

‘Mwanapekee’ wa Rais Samia: Atabadili nini Arusha?

Spread the loveMAPEMA wiki hii, baadhi ya viongozi walioapishwa na Rais Samia...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kipunguni waihoji serikali, ziko wapi fedha za fidia?

Spread the loveWATU wanaodai kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi ni sikivu,...

Habari za SiasaMakala & UchambuziTangulizi

Askofu Bagonza: Tusichonganishwe; tusichokozane na tusikufuru

Spread the loveJOTO la chaguzi linapanda kila siku hapa nchini. Upo umuhimu...

error: Content is protected !!