Monday , 4 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Petroli, diseli, mafuta ya taa sasa ni kitanzi
Habari Mchanganyiko

Petroli, diseli, mafuta ya taa sasa ni kitanzi

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati, Maji na Mafuta (EWURA) imetangaza ongezeko la bei za mafuta ya petroli, diseli na mafuta ya taa, yaliyoshushwa katika bandari ya Dar er Salaam na Tanga. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akitangaza bei za mafuta kwa mwezi Novemba mwaka huu jana jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano EWURA, Titus Kaguo alisema diseli iliyoshushwa katika bandari ya Dar es Salaam imepanga kwa Sh. 81 kwa lita wakati petroli iliyoshuhswa kwenye bandari hiyo ikipanda kwa Sh. 29.

Kaguo alieleza kuwa, diseli iliyoshushwa kwenye bandari ya Tanga imepanda kwa Sh. 111 kwa lita na petroli iliyoshushwa katika bandari hiyo imepanda kwa Sh. 87 kwa lita.

Kufuatia mabadiliko hayo, Kaguo alisema mafuta ya Petroli kwenye mkoa wa Dar es Salaam yatauzwa Sh. 2,396 kwa lita na diseli itauzwa Sh. 2,385.

Aidha, alisema bei ya mafuta yaliyoshushwa katika bandari ya Mtwara imebaki pale pale, kutokana kwamba hakuna mafuta yaliyoingizwa bandarini hapo mwezi uliopita.

Kaguo alisema sababu za bei ya mafuta kupanda ni kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia pamoja na gharama za ucheleweshaji bandarini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

TEF yaomboleza kifo cha Mzee Mwinyi

Spread the loveJukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Maambukizi ya UKIMWI Lindi yapungua

Spread the loveMaambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mgomo kitita kipya cha NHIF: Serikali yaita hopsitali binafsi mezani

Spread the loveSERIKALI imekiita mezani Chama cha Wenye Hospitali Binafsi (APHFTA), ili...

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

error: Content is protected !!