October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru yakwama kuwahoji viongozi ACT-Wazalendo

Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT-Wazalendo

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) imeshindwa kuwahoji viongozi waandamizi wa Chama cha ACT-Wazalendo, kwa kile kilichodaiwa kuwa Ofisa aliyetakiwa kuwahoji hayupo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Viongozi wa ACT-Wazalendo ambao walitakiwa kuhojiwa ni Ado Shaibu Katibu  wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho na Dorothy Temu, Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Leo Tarehe 25 Juni  2019,  viongozi hao waliitwa makao makuu ya Ofisi za Takukuru yaliyokuwepo Upanga jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Viongozi hao waliwasili kwenye Ofisi za Takukuru saa 7 na robo mchana na baadaye saa 8 kamili walielekea ghorofa ya juu kwa ajili ya kusikiliza wito wao ambapo waliambiwa kuwa Ofisa aliyewaita hayupo hivyo wataitwa siku nyingine.

Ado ameiambia MwanaHALISI ONLINE kuwa hadi wakati huu hawajaambiwa lengo la wito huo lakini kutokana na chama chao kimekuwa kikiubua mijadala mbalimbali inayohusu uchumi wa nchi inawezekana ikiwa ni moja ya sababu ya taasisi hiyo kuwaita.

error: Content is protected !!