March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TAKUKURU wamsaka Hans Pope, kisa nyasi bandia

Zakaria Hans Poppe

Spread the love

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imetangaza rasmi kumtafuta aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajiri ya Simba, Zacharia Hans Pope baada ya kutoa taarifa za uongo kwenye ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) juu ya manunuzi ya nyasi bandia za klabu hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Hans Pope alitoa taarifa TRA kuwa Simba ilinunua nyasi kutoka nchini China kwa kiasi cha dola za kimarekani 45,577, sawa na pesa za kitanzania Sh. 105 milioni, kumbe uhalisia walinunua kwa Dola 109,499, sawa na Sh. 252 milioni.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Pregedia Jenerali John Julius Mbungo amesema nia yake ilikuwa ni kutolipa mapata yanayotakiwa na TRA na kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini hilo ni kosa na walijaribu kumtafuta kwa njia ya uwazi ili aje ajibu tuhuma hizo.

“Tumekuwa tukimtafuta kwa njia ya uwazi ‘overt means’ raia huyu mwenzetu haonekana wala hapatikani sisi tunacho mtaka ajitokeze ajibu tu haya mambo yalikuaje yalitokeaje na sheria zipo zitamlinda kama hana hatia,” amesema Mbungo.

Hans Pope ambaye hajaonekana kwa muda mrefu kwenye shughuli za utendaji wa klabu ya Simba bila taarifa yoyote kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo huku Rais wa timu hiyo Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wakishikilia na kesi mahakamani.

error: Content is protected !!