Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC watangaza Uchaguzi mdogo mwingine
Habari za Siasa

NEC watangaza Uchaguzi mdogo mwingine

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage
Spread the love

UCHAGUZI mdogo katika kata 37 za Tanzania Bara unatarajiwa kufanyika tarehe 13 Oktoba 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Tarehe hiyo imetangazwa leo tarehe 14 Septemba, 2018 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage.

Amesema fomu za uteuzi wa wagombea katika uchaguzi wa kata hizo zilizoko katika halmashauri 27 kwenye mikoa 13 ya Tanzania Bara, zitatolewa kati ya  kati ya tarehe 15 hadi 21 Septemba, mwaka huu.

Jaji Kaijage ameeleza kuwa, kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 22 Septemba hadi tarehe 12 Oktoba, 2018.

 “Baada ya kupokea taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za udiwani kwenye kata hizo kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo thelathini na saba (37).”, amesema Jaji Kaijage.

Katika hatua nyingine, NEC imewateua Madiwani watatu Wanawake wa Viti Maalum kujaza nafasi wazi za madiwani katika Halmashauri tatu za Tanzania Bara, akiwemo Halima Salum Kisenga (CCM) wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni.

Na Emmy Anania Shemweta kupitia CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto na Nuru Mwalimu Chuma kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Jaji Kaijage amesema uteuzi huo umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye aliitarifu Tume kuwepo kwa nafasi wazi kupitia vyama hivyo baada ya walioteuliwa kufariki dunia na kujiuzulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!