April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Taasisi za dini kufanyiwa uhakiki

Viongozi wa dini walipokutana na Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

OFISI ya Msajili wa Jumuiya za Kijamii na Taasisi za Kidini, kufanya uhakiki wa taasisi na jumuiya hizo, zilizopo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa tarehe 30 Septemba 2019 na Meja Jenerali, Jacob Kingu, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, zoezi hilo la uhakiki litaanza Oktoba 7 hadi 18 mwaka huu.

“Awamu ya nne ya zoezi la uhakiki itafanyika katika mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Simiyu, Kagera na Shinyanga. Zoezi litafanyika kwenye Kituo cha Uhakiki kilichopo katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni,” inaeleza barua hiyo.

Barua hiyo imeeleza kuwa, wakati wa uhakiki, taasisi na jumuiya husika zinatakiwa kuwa na nyaraka mbalimbali ikiwemo cheti halisi na kivuli cha usajili, stakabadhi ya mwisho ya malipo ya ada iliyolipwa hivi karibuni, katika iliyopitishwa na msajili. Taarifa ya Mkutano mkuu wa mwaka pamoja na taarifa ya fedha ya mwaka.

Barua hiyo imeeleza kuwa, taasisi zitakazoshindwa kuhakikiwa kwa muda uliopangwa zitaondolewa kwenye daftari la msajili.

“Aidha, taasisi za sini na jumuiya za kijamii ambazo hazijasajiliwa zinatakiwa kufika wakati wa zoezi la uhakiki kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kupata usajili,” inaeleza barua hiyo.

 

 

error: Content is protected !!