Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Stars yatoshana nguvu na Congo
MichezoTangulizi

Stars yatoshana nguvu na Congo

Spread the love

 

SARE ya bao 1-1, ilitosha kuifanya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuondoka na pointi moja kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Congo. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo

Fainali hizo zitachezwa nchini Qatar 2022, ambapo kwenye mchezo wa kwanza wa kundi J, uliopigwa nchini Congo, kwenye dimba la TP Mazembe Stars ilitoshana nguvu na wenyeji hao.

Kwenye mchezo huo, Congo walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 22, kupitia kwa Dieumerci Mbokani na dakika 15 baadae Stars walichomoa bao hilo, kupitia kwa Simon Msumva kwenye dakika ya 37, kwa shuti kali nje ya 18.

Stars ambayo ipo chini ya kocha Kim Poulsen iliingia kwenye mchezo huo, huku likikosekana jina la nahodha wake Mbwana Samatta ambaye alichelewa kujiunga na timu hiyo.

Samatta hakulipoti kikosi toka timu hiyo ilipoingia kambini Agosti 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam, na kufanya maandalizi kwa siku tano kabla ya kufasiri Agosti 31 kuelekea nchini Congo.

Kwa matokeo hayo Stars inajiweka kwenye nafasi nzuri ndani ya kundi J, kuelekea mchezo wa pili dhidi ya Madascar utakaopigwa Septemba 7, 2021 kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Stars itarejea nchini kesho kwa ndege ya kukodi ya shirika la ndege la Air Tanzania na kuingia kambini moja kwa moja kujianda na mchezo huo wa Madagascar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

error: Content is protected !!