Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mkurugenzi Temeke aanza kiguu na njia mahakamani
Habari za Siasa

Mkurugenzi Temeke aanza kiguu na njia mahakamani

Spread the love

 

UPELELEZI katika kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke (DED), mkoani Dar es Salaam, Lusubilo Mwakabibi na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP), Edward Haule, kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, haujakamilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 2 Septemba 2021 na Mawakili upande wa Jamhuri, wakiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Mshanga Mkunde, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Evodia Kyaruzi.

Baada ya upande wa Jamhuri kutoa taarifa hiyo, mawakili upande wa utetezi, ukiongozwa na Jeremiah Mtobesya, umeomba upande huo wa mashtaka ukamilishe uchunguzi mapema au iwaache huru washtakiwa kama hauna ushahidi.

Kufuatia hoja hizo, Hakimu Kyaruzi ameahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo hadi tarehe 30 Septemba 2021.

Katika kesi hiyo, Mwakabibi na mwenzake, wanashtakiwa kwa mashtaka mawili ikiwemo la kutumia madaraka yao vibaya kinyume cha Sheria ya Ardhi.

Kufuatia hatua yao ya kuekeleza ujenzi wa stendi ya mabasi, katika kiwanja kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, bila kupewa ruhusa.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2020 na 2021. Kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka, tarehe 20 Agosti 2021.

Mwakabibi na mwenzake, walifikishwa kizimbani kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lililotaka wafikishwe katika mikono ya sheria, kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mkurugenzi huyo wa zamani wa Manispaa ya Temeke, aliondolewa kazini na Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, tarehe 25 Aprili 2021, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!