Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Michezo Stars kucheza bila mashabiki, Nyoni atoa neno
Michezo

Stars kucheza bila mashabiki, Nyoni atoa neno

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Tannzania Taifa Stars italazimika kucheza bila mashabiki kwenye mchezo wao wa pili wa kufuzu fainali kombe la Dunia, dhidi ya Madagascar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa kufuzu fainali kombe la Dunia nchini Qatar 2022, utapigwa kesho majira ya saa 10 jioni, kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari hii leo, Afisa habari wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kuwa, kutokana na muongozo walipewa na Shirikisho la mp[ira wa Miguu ulimwenguni (FIFA), mchezo huo hautakuwa na mashabiki.

“Kutokana na maelekezo tuliopokea kutoka Fifa mchezo wa kesho hautakuwa na watazamaji, kwa hiyo wale waliotalajia kuja uwanja kuinga mkono timu, haitowezekana kutokana na miongozo ya FIFA.” Alisema Ndimbo

Mchezo huo wa kundi J, utakuwa wa pili kwa Taifa Stars mara baada ya kulazimishwa sare kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Jamhuri ya Congo, uliochezwa Septemba 2, mwaka huu kwenye dimba la TP Mazembe, Lubumbashi.

Ndimbo aliendelea kwa kusema kuwa Fifa waliamua kusitisha mashabiki kuingia uwanjani kutokana na mwenendo wa ugonjwa wa UVIKO – 19.

“Fifa wamesema kuwa kutokana na mwenendo wa ugonjwa wa Corona, michezo hiyo haitakuwa na watazamaji, tunaomba watanzania watusapoti huko walipo.”

Kwa upande wa mlinzi wa kati wa timu hiyo, Erasto Nyoni alisema kuwa, wao kama wachezaji hawajapokea vibaya taarifa hiyo ya kutoudhulia kwa mashabiki Uwanjani, na hivyo wao kama wachezaji wamejiandaa kucheza mchezo wa kesho.

“Moja ya motisha yetu ni kuingia kwa mashabiki ndani ya Uwanja, lakini sisi hatujaipokea vibaya taarifa hiyo, sisi tumejiandaa kucheza mchezo wa kesho, tunaamini hata mkiwa nje ya Uwanja mtatupa ushirikiano” Alisema mchezaji huyo

Ikumbukwe Madagascar wanaingia kwenye mchezo huo, huku wakitoka kupoteza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Benin.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!