Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Askofu Shoo alalamikia tozo, akumbuka upinzani bungeni
Habari Mchanganyiko

Askofu Shoo alalamikia tozo, akumbuka upinzani bungeni

Spread the love

 

MJADALA juu ya tozo mbalimbali zilizoanzishwa na serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kupeleka maendeleo ya haraka kwa wananchi, bado ungali moto na kwamba zaweza kuwa mwiba katika uchaguzi mkuu ujao. Anaripoti Gift Mongi, Moshi … (endelea).

Akizungumza kanisani kwake jana Jumapili tarehe 5 Septemba 2021, Askofu Mstaafu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Jimbo la Kilimanjaro, Dk. Glorious Shoo alisema, tozo hizo, ni madhara ya Bunge kuwa la uwakilishi mkubwa wa chama kimojaa (Chama Cha Mapinduzi – CCM).

Alisema, kukosekana kwa mawazo mbadala bungeni, kumechangia kwa kiasi kikubwa, kuwapo kwa malalamiko juu ya tozo na kodi nyingine, kwa kuwa jambo hilo, halikuweza kujadiliwa kwa kina bungeni.

“Haya ni matokeo ya Serikali kukosa mawazo mbadala kutoka upinzani. Mara nyingi mawazo ya wapinzani yalikuwa na mchango mkubwa kwa jamii na taifa,” alieleza Askofu huyo mstaafu.

Alisema, kuwapo kwa upinzani bungeni, ilikuwa ni njia sahihi ya watu wenye mawazo mbadala, kupata sehemu ya kusemea, lakini Serikali ilivyotumia nguvu kuua upinzani, ndipo wananchi wakakosa kutoa mawazo yao mbadala.

“Binafsi sina shida na tozo, sijui LUKU, shida kubwa iliyopo hapa, ni kuwa upinzani umeondolewa bungeni, ambao kwa kiasi fulani ulikuwa na mawazo mbadala. Kwa sababu, ukiangalia hata hizo tozo, sidhani kama kuna utafiti uliofanyika,” ameeleza Askofu Dk. Shoo.

Hata hivyo, pamoja na lengo la kuanzishwa tozo hiyo kuwa jema, yameibuka malalamiko katika maeneo kadhaa kutoka kwa wananchi wakisema, tozo zilizoanzishwa ni kitanzi kwao, kutokana na kile wanachoeleza kuwa ni kukauka kwa mifuko yao.

Wakati Dk. Shoo akitoa kauli hiyo, Chama cha ACT-Wazalendo, kimetaka serikali kutafuta vyanzo vingine vya mapato, ili kuachana na tozo wanazodai kuwa zinawaumiza wananchi wa kipato cha chini.

Akichambua tozo hizo, Askofu Dk Shoo alisema, kukosekana kwa mawazo mbadala nchini, matokeo yake kukumbatiwa kwa mawazo ya upande mmoja (chama tawala), “jambo ambalo hata kama linaumiza wananchi, linapitishwa bila kuhojiwa na kuangaliwa kwa kina.”

Alisema, “mimi ni Mchungaji na hapa nikitaka mambo yaende sawa, nikichagua wazee wa Kanisa siwezi kuchagua ambao wanaitika kila ninalosema. Ni lazima niwaweke na wale ambao wananipinga, ili nikichanganya mawazo yao, napata njia sahihi.”

Alisema kama Serikali inataka kwenda mbali zaidi, itafute njia ya jinsi ya kukutana na vyama vya upinzani, ili kupata mawazo mbadala, tofauti na sasa ambako hakuna anayewaza mbali zaidi na hiyo ndiyo maana halisi ya upinzani.

“Nikisema wapinzani wanasaidia, naonekana kuwa na mimi ni mpinzani, ila ukweli wangekuwapo bungeni, wangekuja na mawazo mbadala na tungekuwa katika hatua nzuri zaidi. Hakuna mtu anayekataa kulipa kodi, shida ni jinsi jambo lenyewe lilivyokaa,” alifafanua Askofu mstaafu Dk. Shoo.

Askofu Dk. Shoo ambaye pia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kilimanjaro International Christian Centre (KICC), alieleza kukosekana kwa wapinzani wa kuwasemea wananchi bungeni, kumesababisha wananchi kubaki kuwa wapinzani, jambo ambalo zuri kwa afya ya taifa.

Alisema, nchi nyingi zilizojaribu kuua upinzani, mambo hayakwenda vizuri na kwingine kuharibika kabisa.

“Namshauri Rais Samia, afanye jitihada za makusudi za kukutana na upinzani na aweze kupata kutoka kwao jambo ambalo pia litamwezesha kuendesha nchi kirahisi. Hawa ni Watanzania wenzake na wana mchango wao wa mawazo, hivyo akichukua yao na yake, ataendesha nchi bila nguvu,” alisema Dk. Shoo.

Kuhusu kodi alisema, Askofu huyo alisema, si kwamba wananchi wanakataa kulipa, bali ni jinsi inavyoletwa kwao, bila hata kuhojiwa na kufanyiwa utafiti wa kina.

Tozo zinazolalamikiwa kwa sasa, ni pamoja na zile zinazotolewa kwenye miamala ya simu za mkononi ambazo hivi karibuni Serikali imetangaza kuzipunguza kwa asilimia 30 huku makampuni ya simu yakipunguza asilimia 10 ili kumuondolea maumivu mwananchi.

Kodi zingine zinazolalamikiwa, ni tozo ya majengo, ambayo inalipiwa kupitia ununuaji wa umeme kwa njia ya LUKU, ambako sasa hata wapangaji wanalazimika kulipia kwa maelezo kuwa “wao ndio wanaopaswa kuelewana na wenye nyumba.”

Tozo nyingine, ni ile inayotozwa kupitia mafuta ya taa, diseli na petrol, ambazo zimesababisha bidhaa hizo kupanda na kuibua malalamiko kutoka kwa wananchi.

Kwa mfano, kodi ya mafuta ya taa inatajwa kuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi waishio vijijini ambao wengi wao ni maskini, na inasababisha uhalibifu wa mazingira, kufuatia wananchi wengi, kikimbilia matumizi ya mkaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!