October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

STAMICO yatoa gawio la Sh 2.2/- ikiahidi makubwa

Spread the love

 

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa gawio kwa Serikali kiasi cha Sh 2.2 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/21 huku wakitarajia kuongeza zaidi kwa mwaka 2022/23. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Pamoja na kutoa gawio hilo shirika hilo limeeleza kuwa kwa sasa limejipambanua baada ya kuomba pesa serikalini linarudisha pesa serikalini kwa kutoa gawio.

Akitoa taarifa ya Shirika hilo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Stanico Dk. Venance Mwasse leo tarehe 12 Agosti 2022 kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO amesema kuwa shirika hilo kwa sasa pamoja na changamoto za uhaba wa watumishi na sheria ya manunuzi bado wanajitahidi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi.

Aidha ameeleza kuwa kwa kuhakikisha Shirika linafanya vizuri na kurejesha fedha serikalini badala ya kuomba pesa serikalini katika mwaka wa fedha 2022/23 wanakusudia kutoa gawio la Sh. 5 Bilioni.

Akizungumzia mafanikio Dk. Mwasse ameeleza kuwa Shirika limeweza kufufua mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira na kuweza kupata tani 60,000 ambazo usafirishwa nje kila mwezi na kuingiza fedha kiasi cha Sh4.12 bilioni kila mwezi.

Aidha ameeleza kuwa katika kuendelea kuboresha mgodi huo bado wanakusudia kupata tani laki moja kila mwezi ambapo itaongeza mapato.

Aidha ameeleza kuwa katika kuendelea kuboresha sekta ya wachimbaji wadogo imenunuliwa mitambo mikubwa 10 kwa ajili ya uchimbaji mdogo ili waweze kufanya utafiti wao wenyewe.

error: Content is protected !!