October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mawakala Ruto, Odinga wazozania kifaa cha majumuisho ya kura

Spread the love

WAANDISHI wa habari wamelazimika kutolewa katika kituo kikuu cha majumuisho ya kura za urais cha Bomas kupisha majadilino ya maafisa wa Tume Huru na Mipaka ya Uchaguzi (IEBC) na mawakala wa Azimio na UDA kufuatia mzozo ulioibuka baina yao. Vyombo vya ndani nchini humo vimeripoti.

Kwa mujibu wa tovuti ya Daily Nation mawakala hao wamezozana kuhusu madai ya kifaa cha majumuisho ya kura kutiliwa shaka kuingizwa ndani ya chumba hicho madai yaliyotolewa na mawakala wa Azimio.

Upande wa Azimio umegomea uwepo wa kifaa hicho ambacho bado hakijatambuliwa na kusababisha kusitishwa kwa mchakato wa uhakiki wa kura.

error: Content is protected !!