Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko STAMICO, BUCKREEF yawapiga msasa wananchi, wachimbaji wadogo Geita
Habari Mchanganyiko

STAMICO, BUCKREEF yawapiga msasa wananchi, wachimbaji wadogo Geita

Spread the love

SHIRIKA la  Madini la Taifa (STAMICO) kwa kushirikiana na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Buckreef Gold wametoa elimu kuhusu uchimbaji wa madini na umuhimu wake katika jamii kwa wananchi waliotembelea migodi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Elimu hiyo imetolewa wakati wa ziara ya washiriki wa maonesho ya tano ya madini waliokwenda kutembelea migodi hiyo miwili  na kujionea jinsi inavyotoa fursa kwa vijana wa Tanzania  iliyoandaliwa na waandaji wa Maonesho ya Tano ya kitaifa ya Teknolojia Madini yanayoendelea mkoani Geita.

 

Akitoa elimu  ya uchimbaji  mdogo Msimamizi  wa Kituo cha Mfano cha wachimbaji wadogo,  Mhandisi migodi Victor Olal amesema STAMICO inasimamia shughuli za uchimbaji madini sambamba na kuendesha mafunzo ya uchimbaji  kwa vitendo ili kuhakikisha  wachimbaji wadogo wanafanya uchimbaji wenye tija na manufaa.

Amesema kupitia vituo hivyo STAMICO imewazesha  wachimbaji  kuelewa umuhimu na kutumia  teknolojia ya kisasa katika uchimbaji hivyo kupelekea baadhi ya wachimbaji wadogo kuwa na shauku ya kutumia tekinolojia hiyo katika maeneo yao.

“Ni jambo la kujivunia kuona wachimbaji wadogo wengi wameanza kuelewa na kuthubutu kutumia teknolojia hii, kwani hadi sasa baadhi ya wachimbaji wameanza kujenga mitambo ya uchenjuaji inayofanana na hii” ameongeza Olal.

Amesema kupitia sekta ya uchimbaji mdogo vijana wengi wanapata fursa ya ajira, kujifunza uchimbaji wa kisasa, biashara hata kujipatia maendeleo binafsi.

 

“Vituo hivi hutoa ajira kwa watu wengi wazawa, vinatumia teknolojia ya kisasa hivyo kupunguza athari zinazotokana na kemikali hatarishi kama zebaki”

Ziara hii pia imetoa fursa kwa washiriki kutembelea shughuli za uchimbaji mkubwa na kujionea jinsi dhahabu inavyopatika kuanzia hatua za  utafiti, uchimbaji na uchakataji  wake katika  mgodi wa Buckreef  Gold

Aidha, wameona manufaa ya mgodi huu kwa watanzania ikiwemo ajira, uwajibikaji katika huduma za kijamii zikiwemo, hospitali, shule na miundombinu ya barabara.

Mhandisi Mwandamizi wa Migodi, Erick Yohana amefafanua kuwa kampuni ya Buckreef inafanya kazi kwa weledi katika kila kada  na kuendeshwa kwa 100% ya waajiriwa watanzania.

Amesema kampuni hiyo inazidi kujiongezea uwezo wa uzalishaji jambo litakalopelekea kuongezeka  kwa fursa za ajira kwa Watanzania.

Vilevile, Mgodi wa Buckreef unafanya kazi na wazabuni na wakandarasi wa Kitanzania katika kupata bidhaa na huduma.

Ameongeza kuwa shughuli za uchimbaji mgodini hapo huzingatia sana suala la usalama wa watu, vifaa, na vyote vinavyozunguka mgodi huo.

Kutembelea migodi hiyo miwili  kumewawezesha washiriki hao kutofautisha uchimbaji mkubwa na uchimbaji mdogo na kujionea umuhimu wa kila mmoja katika jamii na Serikali kwa ujumla.

Aidha, mmoja washiriki katika ziara hiyo, Kelvin Haule ametoa pongezi kwa STAMICO pamoja na Buckreef kwa kutoa fursa kwa watanzania ya kusimamia shughuli za uchimbaji katika migodi hiyo na kutoa nafasi kwa wageni mbalimbali kujionea na kujifunza.

Aidha, ametoa pongezi kwa kamati ya kuratibu Maonesho ya Tano  ya Madini kwa kuandaa ziara katika migodi mbalimbali ili kuangalia sekta ya madini inavyotoa fursa za ajila na Maendeleo kwa jamii ya wa watanzania.

Washiriki wa maonesho ya Madini wametembelea katika Mgodi wa Buckreef na kituo cha mfano cha wachimbaji wadogo chenye mgodi na mtambo wa kuchakata dhahabu  ili kujionea shughuli mbalimbali za uchimbaji na kuweza kutofautisha aina za uchimbaji madini  unaofanyika  nchi ikiwemo uchimbaji mkubwa wa kati na uchimbaji mdogo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!