Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Spika Tulia aeleza sababu za kengele ya hatari kulia Bungeni

Spika Dk. Tulia Ackson
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amesema kengele ya hatari iliyofanya mhimili huo usitishe shughuli zake kwa muda, imetokana na marekebisho yaliyokuwa yanafanywa katika sehemu ya chini ya ukumbi wake, yaliyosababisha vumbi na kupelekea mifumo ya usalama kuhisi kuna moshi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Spika Tulia ametoa taarifa hiyo leo Jumanne, muda mfupi baada ya kikao cha Bunge kurejea.

“Hitilafu imetokana na kwamba walikuwa wanafanya marekebisho ilidi watindue eneo, katika kutindua vumbi ikatoka na vinavyonasa hitilafu ikanasa ile vumbi kama moshi. Kwa hiyo ndiyo maana ikapiga kelele kuashiria kuna shida kwenye jengo hili,” amesema Spika Tulia.

Spika Tulia amewatoa hofu wabunge na wananchi kwamba changamoto hiyo imedhibitiwa na kwamba marekebisho yanaendelea kwa utaratibu mzuri.

Kengele ya dharura ililia wakati Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, anajibu maswali ya wabunge. Ambapo Spika Tulia aliahirisha kikao hicho kwa muda na kuwataka wbaunge watoke nje ya ukumbi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!