Spread the love

 

ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania, Sophia Simba amekuwa miongoni mwa. Wanachama 17 wa chama hicho, kuchukua fomu ya kuwania uspika wa Bunge wan chi hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Sophia aliyewahi kuhudumu wizara mbalimbali katika utawala wa awamu ya nne wa Jakaya Kikwete, amechukua fomu leo Jumanne, tarehe 11 Januari 2022, ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Job Ndugai aliyejizulu, imeanza jana Jumatatu 10 hadi 15 Januari 2022.

Akizungumza Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, Solomon Itunda Katibu msaidizi mkuu idara ya oganizesheni amesema leo Jumanne Ofisi kuu ya CCM, Dodoma waliochukua fomu ni watatu na Ofisi ndogo ya Lumumba Dar es Saalam ni watano na kufikisha jumla ya wanachama 17 yangu mchakato uanze jana Jumatatu.

Kati ya waliochukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika ni pamoja na mwanasiasa mkongwe ndani ya siasa za CCM na ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM (UWT) pamoja na kushika wadhifa mbalimbali Sophia Simba.

Itunda amewataja waliochukua fomu ya kugombania nafasi ya usipika katika ofisi ndogo ya Lumumba Jijini Dar es salaam kuwa ni Joseph Msukuma, Goodluck Ole-Madeve, Sophia Simba.

Amewataja wengine kuwa ni pamoja na Juma Chum,Baraka Byabato,Musaa Zungu Emmanuel Mwakasaka na Prof. Handley Mafwenga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *