Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli
Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Sheikh Mussa Kundecha, aliyekuwa Amiri wa Shura ya Maimamu nchini Tanzania
Spread the love

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai imevunja ahadi yake ya kuwapa umiliki wa mitaala ya somo la elimu ya dini ya kiislamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Lawama hizo zimetolewa leo tarehe 27 Septemba 2023, jijini Dar es Salaam na Amir wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Mussa Kundecha, akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Jopo la Wataalamu wa Kiislamu, linaloundwa na jumuiya hiyo.

Sheikh Kundecha alidai kuwa, katika vikao tofauti tofauti ambavyo wameketi na uongozi wa Wizara ya Elimu, akiwemo Waziri Prof. Adolph Mkenda, kwa ajili ya kuandaa na kuratibu ufundishaji wa dini ya Kiislamu na lugha ya Kiarabu, Serikali iliahidi kuacha umiliki wa somo hilo kwa waislamu, lakini mwisho wa siku imeshindwa kutekeleza ahadi hiyo.

“Kinachotutia wasiwasi ni kwamba, katika kikao cha tarehe 12 Agosti 2023, Prof. Mkenda aliomba radhi na kukiri suala hili la umiliki wa mtaala libaki kwa waislamu wenyewe kwamba michakato yote kwenye hili TET wasiingilie,” amesema Sheikh Kundecha.

Sheikh Kundecha amedai “wakati vikao na michakato yote ikiendelea, kuna mambo yanatatiza bado, hadi sasa ukitembelea tovuti ya Taasisi ya Elimu Tanzania kwenye kiunga cha mitaala, mihutasari na moduli, ipo mihutasari ya ya masomo 15 ya dini haijawekwa sababu TET haina haki miliki.”

“Lakini cha ajabu katika mihutasari ya elimu ya sekondari upo wa somo la elimu ya dini ya kiislamu ambayo imeeleza haki miliki yote ni ya serikali hadi kudurufu ni kosa kisheria bila kupata idhini ya maandishi,” amedai Sheikh Kundecha.

Kufuatia malalamiko hayo, MwanaHALISI Online uliitafuta Wizara ya Elimu, kwa ajili ya kupata ufafanuzi wake, ambayo imekanusha madai hayo ikisema haijachukua haki miliki ya mitaala hiyo.

Aidha, wizara hiyo imedai jumuiya hiyo imetafsiri vibaya baadhi ya mambo, huku ikiahidi kutoa ufafanuzi wa kina pindi itakapopitia kwa ufasaha madai hayo.

1 Comment

  • Ni Uislamu gani utakaofundishwa? Kwani kuna Waislamu wa firka au madhenebu mbali mbali kama vile Shia, Sunni, Shafi, Hambali, Ibaadhi, Hanafi, Maliki, Deobandi, Ismailiya, Sufi na kadhalika . Pia kuna na Ahmadiya
    Wote hawa watadai watoto wao wafundishwe imano yao. Vurugumechi. Ni vizuri ufundishaji wa dini uwe nje ya mtihani wa wizara na uwe suala la binafsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!