Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Sita wafariki dunia ajali iliyohusisha Noah na lori Arusha
Habari Mchanganyiko

Sita wafariki dunia ajali iliyohusisha Noah na lori Arusha

Spread the love

 

WATU sita (06) wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la Alkatani kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema ajaili hiyo ilitokea tarehe jana tarehe 19 Aprili, 2022 muda wa saa nne usiku.

Ameyataja magari yaliyohusika kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea Makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva amabapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Kamanda Masejo amesema kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kufamu majina halisi ya abiri waliofariki katika ajali hiyo na amewaomba wananchi kufika katika hosptali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru kutambua miili ya marehemu.

ACP Masejo ametoa wito kwa watumiaji wa vyombo vya moto kuwa waangalifu wakati wamatumizi ya vyombo hivyo ilikupunguza ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!