Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Simbachawene akumbushia machungu ya siasa za kipindi cha nyuma
Habari za Siasa

Simbachawene akumbushia machungu ya siasa za kipindi cha nyuma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene
Spread the love

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), George Simbachawene, amevitaka vyama vya siasa kufanya siasa za kistaarabu ili kuepusha vitendo vinavyohatarisha amani na utulivu wa nchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, tarehe 5 Januari 2023, akizungumzia ruksa ya mikutano ya hadhara iliyotolewa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan, katika mkutano wa mtandaoni, uliondaliwa na Taasisi ya Watch Tanzania.

Waziri huyo amedai kuwa, huko nyuma katika siasa za Tanzania, watu waliumizana, baadhi walipoteza maisha huku wengine wakipoteza viungo vyao, kutokana na ukosefu wa siasa za kiustaarabu.

“Siasa za kistaarabu ni zile zinazoweza kufanyika kama mikutano au chochote kile bila kusababisha uvunjifu wa amani kama kupigana na mambo kadhaa. Utakumbuka huko nyuma katika siasa za nchi yetu watu waliumizana sana, wako waliokufa, waliotiwa vilema, wako waliomwagiwa tindikali, hizo sio siasa huo ni unyama sababu wako watu wamepoteza viungo,” amesema Simbachawene.

Simbachawene amesema “wako watu namna ambavyo walikashifiwa na kusingiziwa mambo ilikuwa inatishia hata amani sababu kinachoanza ni maneno, baadae inakuja vitendo vya uvunjifu wa amani.”

Amesema, siasa za kistaarabu zinasaidia hata vyama vya upinzi kujiimarisha na kuungwa mkono na wananchi “naamini katika siasa za kistaarabu kuna ujenzi wa itikadi ya chama chako kuliko siasa za matusi, kashfa, fujo na mapigano. Nakumbuka wakati vyama shindani vilipata kujijenga  wakati wa masuala ya ufisadi ambao ulikuwa unaibuliwa ndani na nje ya Bunge.”

Akizungumzia hatua ya Rais Samia kuondoa zuio la kufanya mikutano ya hadhara, Simbachawene amesema wizara yake imejipanga kulisimamia vyema suala hilo na kwamba imeboresha taratibu za mikutano hiyo kufanyika, huku akivitaka vyama vya siasa vya upinzani kutekeleza maagizo ya mkuu huo wa nchi kwa kufanya siasa za kistaarabu.

“Tutaendelea kufanya kazi yetu katika hali bora zaidi sababu tunaamini yale yaliyoelezwa na Rais Samia wenzetu wameyasikia na wanaweza kuyazingatia na hivyo tukajenga demokrasia ambayo imepevuka, nchi yetu sasa ni kubwa ina uzoefu katika demokrasia,” amesema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene amesema Serikali ya Awamu ya Tano, chini ya Hayati John Magufuli, ilipiga marufuku ya mikutano ya hadhara kwa muda ili kukwepa athari za vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa 2020, ambapo baadhi ya vyama vilitaka kuingia barabarani kupinga matokeo huku vingine vikitaka kufanya maandamano kwa ajili ya kushukuru wananchi kwa kuwapa kura nyingi.

“Marufuku haikuja tu, ilikuja baada ya kuona kuna matokeo hasi kwa maana ya stability ya nchi. Tumemaliza uchaguzi Serikali iliyochaguliwa na wananchi inaingia kazini kutekeleza iliyoahidi na inapaswa kupata utulivu wa kufanya hivyo,” amesema Simbachawene na kuongeza:

“Ilitokea mzingira yale sababu kidogo vuguvugu la uchaguzi linapokuwa moto wake mkali , vyama vilitaka kuingia barabarani kama ilivyoelezwa kuna vyama vilitaka kwenda kutoa shukrani kwa kupata kura, kuna vyama vinataka kwenda kusema hatukubaliani na matokeo. Basi hii nchi maana yake isingetawalika.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!