Tuesday , 21 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Simbachawene aingilia kati mgogoro NCCR-Mageuzi
Habari za SiasaTangulizi

Simbachawene aingilia kati mgogoro NCCR-Mageuzi

Spread the love

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, George Simbachawene, ameitaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kushughulikia mgogoro ndani ya Chama cha NCCR-Mageuzi kwa kuzingatia katiba ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hayo yameelezwa leo tarehe 28, Agosti, 2022 na Samweli Ruhuza Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho upande unaomuunga mkono Mwenyekiti James Mbatia ambaye amesimamishwa.

Ruhuza amesema Sambachawene amemwandikia Msajili wa Vyama vya Siasa barua ya tarehe 15, Agosti 2022 kumtaka amalize mgogoro huo uliokigawa chama vipande viwili upande mmoja ukiongozwa na Katibu Mkuu Martha Chiomba na upande mwingine Menyekiti Mbatia.

????????????????????????????????????

Pande zote mbili zimekuwa zikituhumiana na kusimamishana uongozi ambapo upande wa Mbatia umemsimamisha kazi Chiomba huku kwa upande wake ukimsimamisha kazi Mbatia.

Hata hivyo, Ruhuza ameituhumu Ofisi ya Msajili kuchochea mgogoro huo ikiwemo kuhushi nyaraka za chama hicho kusukuma ajenda zake na kuhudhuria vikao vya upande mwingine ambao amedai si halali kwasababu hauna akidi.

“Simbachawene aliandika barua tarehe 15 mwezi wa nane kwa msajili akimtaka amalize tatizo linaloitwa mgogoro ndani ya NCCR-Mageuzi na akampa vitu vbya kuvianagalia akamwelekeza kuangalia katibaya chama kanuni za chama vikao vilivyoitishwa na chama na kuweka haki katika kutatua tatizo hilo ambalo linaitwa mgogoro,” amesema na kuongeza;

“Huyo aliyeandika ni Waziri lakini mpaka leo Msajili kimya. Hajafanya kitu chochote, sasa tunajiuliza ana nia gani na NCCR-Mageuzi mbona amekuwa mzito? Amehoji.

Ruhuza ameenda mbali zaidi na kumtaka Rais Samia Suluhu Hassan kujitafakari kuhusu ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kushindwa kutekeleza majukumu yake kinyume na sera yake ya kutaka kudumisha amani, upendo, haki na mshikamano wa kitaifa.

“Ofisi ya msajili inafanya tofauti na sera yake na Rais amekaa kimya wakati ofisi ya msajili inaleta mtafaruku unashindwa kuelewa huyu Rais Samia Sulhhu hassan ni mkweli kwenye kauli zake?”

“Tulitegemea hawa wanavyofanya uhuni Rais awe ameshituka kwasababu ana vyombo vingi vya kufuatilia na kumpa taarifa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Watumishi 25,039, taasisi 65 wahamia Dodoma

Spread the loveSerikali imesema hadi sasa, jumla ya watumishi 25,039 kutoka Serikali...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the loveKatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Habari za SiasaKimataifa

Kiongozi Mkuu Iran amteua mrithi wa Rais Ebrahim

Spread the loveKiongozi wa ngazi ya juu nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei,...

error: Content is protected !!