Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaufadhili mfumo wa Diaspora
Habari Mchanganyiko

NMB yaufadhili mfumo wa Diaspora

Spread the love

BENKI ya NMB na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wamesaini Hati ya Makubaliano (MoU), ambapo NMB itafadhili Matengenezo ya Mfumo wa Utunzaji wa Taarifa za Diaspora Kidijitali (Diaspora Digital Hub System), kwa kiasi cha Sh100 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Makubaliano hayo yamesainiwa Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, ambako Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Arika Mashariki, Balozi James Bwana, alimwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Joseph Sokoine.

Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana (kulia) na Afisa Mkuu wa wateja wakubwa na Serikali,wa Benki ya NMB, Alfred Shao wakibadilisha hati baada ya kutiliana saini ya makubaliano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB kwa ajili ya ufadhili wa matengenezo ya Mfumo wa Kidigitali wa kutunza Taarifa za Diaspora wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Balozi Bwana ameishukuru NMB kwa kukubali kutoa ufadhili wenye thamani ya Sh.100 milioni, unaoenda kufanikisha matengenezo ya mfumo huo, ambao utakapokamilika utawatambua, kuwasajili na kutunza data za Diaspora wa Tanzania waliotapakaa duniani kote kupata huduma muhimu.

Amesema mfumo huo ambao utakamilika na kuanza kazi kabla ya Desemba 2022, utakuwa chachu ya ushiriki wa Diaspora wa Kitanzania kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, kibiashara, kiuchumi na kiuwekezaji nchini, licha ya umbali waliopo.

“Matumaini yetu ni kukamilisha mfumo kabla ya mwisho wa mwaka huu na kimsingi unaenda kuiwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za idadi ya Diaspora wetu, huku ukibeba faida mbalimbali, ikiwemo kuwaunganisha, kuwashirikisha na kuwahamasisha wao kupata huduma kimtandao.

“Aidha, mfumo huu utawezesha kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kuhamasisha taasisi mbalimbali nchini kuwekeza katika kidijital ili kuongeza tija ya matumizi ya sahihi ya muda wa wanaohudumiwa na kupunguza urasimu, sanjari na kuiwezesha wizara kwenda sambamba na dunia katika teknolojia,” amesema Balozi Bwana.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Alfred Shao, aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Ruth Zaipuna, ameipongeza Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuthamini mchango wa NMB na kuamua kuwashirikisha katika mchakakato wa matengenezo ya mfumo huo.

Shao amesema, makubaliano hayo ni muhimu kwa ustawi wa taifa na maendeleo ya Diaspora na kwamba Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni muhimu sana katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya taifa na kwa kutambua hilo, NMB haikusita kufadhili matengenezo ya mfumo huo.

“NMB tukiwa ni washirika wakubwa wa maendeleo ya taifa, tunakoshirikiana vema na Serikali katika uanzishwaji wa mifumo mbalimbali ya kidijitali, hasa ukizingatia tunayo Idara ya Diaspora iliyosheheni wataalamu na masuluhisho mengi ya Diaspora, tukaona tushiriki hili kwa kutoa ufadhili wa matengenezo haya.

“Tunatoa Sh.100 milioni kufanikisha kuandaa na hatimaye kutumika haraka kwa mfumo huu muhimu. Tunaipongeza Wizara na kuwahakikishia kuwa jambo linalofanyika hapa leo ni kwa manufaa ya Taifa na Watanzania waliopo nje ya nchi. NMB tumejipanga vya kutosha kuwahudumia Diaspora popote walipo,” amesema Shao.

1 Comment

  • Kama Diaspora wanaoishi nje ni muhimu kwa maendeleo yetu kwanini hatuwapi aina fulani ya uraia pacha kama wafanyavyo huko India ambako wanapewa non-residential Overseas Indian citizenship?

    Pili, kwanini wastaafu wanalazimishwa kupokea malipo yao kupitia NMB? Kwanini pensheni yao wasiweze kujichagulia benki waipendayo? Si mmeruhusu ushindani wa benki? Sasa why monopoly kwa NMB???

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua bima ya afya kwa wakulima

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na kampuni...

Habari Mchanganyiko

Makamba awasili China kwa ziara ya kikazi

Spread the loveWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Ethiopia yafungua njia ujenzi wa ubalozi Dodoma

Spread the loveSerikali ya Tanzania imeipongeza Serikali ya Ethiopia kwa kuweka historia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Total Energies yawekeza bilioni 17 kusambaza gesi ya kupikia

Spread the loveILI kurahisisha upatikanaji wa gesi ya kupikia kwa gharama nafuu...

error: Content is protected !!