Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Simba yataka Yanga ishushwe daraja
Michezo

Simba yataka Yanga ishushwe daraja

Spread the love

KLABU ya Simba imelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuishusha daraja Yanga kwa kugomea mchezo wao wa jan0a wa Ligi Kuu Tanzania namba 208 u,liopaswa kucheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Yanga waligomea mchezo huo baada taarifa ya mabadiliko ya muda kutoka TFF na kutaka mchezo kuchezwa saa 1 usiku badala ya saa 11 kama ulivyopangwa awali.

Taarifa iliyotolea na klabu ya Simba imeeleza kuwa kitendo kilichofanywa na klabu ya Yanga tafsiri yake ni kugomea mchezo na wanapaswa kushushwa madaraja matatu na Simba kupewa ushindi wa pointi tatu.

Aidha taarifa hiyo ilikwenda mbali na kueleza kuwa baada ya kupewa taarifa ya muda wa mabadiliko ya mchezo wenzao Yanga walikubali lakini wanashangaa kwa nini mchezo huo ulihailishwa.

Katika hatua nyingine Simba imesema kuwa kuhailishwa kwa mchezo huo ni mpango wa Bodi ya Ligi kuipendelea Yanga ambao walipaswa kutii maelekezo.

Klabu hiyo pia imeamua kuchukua maamuzi ya kuziandika barua mamlaka husika ili kupata ukweli wa jambo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!