Saturday , 10 June 2023
Home Kitengo Michezo Simba yamtimua kocha wa Azam FC
Michezo

Simba yamtimua kocha wa Azam FC

Hans Van der Pluijm (wa nyuma) akiwa na msaidizi wake Juma Mwambusi walipokuwa katika majukumu yao katika kikosi cha Azam FC
Spread the love

KIPIGO cha mabao 3-1 waliofungwa na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kimesababisha klabu ya Azam FC kuachana na kocha wake, Hans Van Pluijm pamoja na msaidizi wake Juma Mwambusi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Uongozi wa klabu hiyo umeamua kuchukua maamuzi hayo kufuatia timu hiyo kutopata matokeo katika michezo mitano mfululizo kwenye Ligi Kuu baada ya kufungwa michezo miwili dhidi ya Simba na Prisons na kwenda sare kwenye michezo dhidi ya KMC, Alliance na Coastal Union.

Baada ya kufungushiwa virago leo, kocha huyo amewashukuru mashabiki wa timu hiyo pamoja na kuwatakia mafanikio mema hasa kwa kocha afuatae na alimaliza kwa kusema kuwa kocha anaajiliwa ili afukuzwe.

“Asanteni mashabiki wa Azam FC ambao siku zote hata kwenye kipindi kigumu mlikuwa nyuma yangu mkinisapoti.

“Namtakiwa mafanikio mema kocha ajaye, nimekuwa na wakati mzuri Azam FC na nilijitahidi kadri niwezavyo ili kufikia malengo ya klabu lakini ndiyo hivyo, naamini atakayekuja ataendeleza kile nilichofanya,” alisema kocha huyo.

Toka timu hiyo ipande daraja 2007 timu hiyo imetimua jumla ya makocha 12 pamoja na Stewat Hall ambaye ameinoa timu hiyo katika vipindi vitatu tofauti.

Makocha mpaka sasa waliotimuliwa na Azam katika kipindi cha miaka 12 ni Mohammed King (Zanzibar), Neider dos Santos (Brazil), Itamar Amorin (Brazil), Boris Bunjak (Serbia), Joseph Omog-Cameroon, George Nsimbe (Uganda), Zeben Hernandez (Hispania), Idd Nassor Chechen a Hans Van Pluijm.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

HabariMichezo

Benki ya NBC yazindua kombe jipya la Ligi Kuu Tanzania Bara

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa Ligi ya NBC , Benki ya Taifa...

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Michezo

Samia aipongeza klabu ya Yanga kwa hatua iliyofikia

Spread the love RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

error: Content is protected !!