March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ashtukia ufisadi wa Mil.100 soko la Manzese

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo (mwenye fulana ya bluu na nyekundu) akikagua machinjio ya kuku katika soko la Manzese

Spread the love

ZIARA  ya Saed Kubenea Mbunge wa Jimbo la Ubungo amebaini ufisaidi wa Sh. 100 milioni kwenye machinjio ya kuku kwenye soko la Manzese. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kubenea leo tarehe 23 Februari amefanya ziara kwenye kata hiyo kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi iliyotekelezwa na jimbo lake.

Kubenea amefika Ofisi ya Kata ya Manzese na baadaye aliondoka na viongozi wa kata wakiambatana na mwenyeji wake Ramadhan Kwangaya Diwani Kata hiyo.

Mbunge huyu ametembelea kwenye uwanja wa Manzese ambapo watumiaji wa uwanja huo wanamuomba kuukarabati uwanja huo.

Kubenea aliyekuwa akitembea kwa miguu mtaa kwa mtaa huku akiwasalimu wananchi amekwenda kwenye soko la Manzese.

Mbunge huyo amefika kwenye machinjio hayo ambapo alikutana na Mwenyekiti wa Soko hilo Hamis Mgana aliyemueleza wafanyabiashara kwenye soko hilo wapo kwenye mazingira mabovu ya kufanya biashara zao.

Hamis Mgana amemueleza Kubenea kuwa kwa sasa wafanyabiashara wa machinjio hayo wapo kwenye mazingira magumu licha ya kuwa lipo jengo lililojengwa kwa kandarasi ya Manispaa ambapo hadi sasa wanaoupungufu wa wazi kwenye ujenzi huo.

Mgana  amesema kuwa zipo kila dalili kuwa jengo hilo limejengwa kwa kiwango cha chini ingawa wameambia kuwa jengo hilo limegharimu Sh. 92 milioni.

Ametaja moja ya kasora za jengo hilo  ni kutokuwa chemba kubwa za maji, jengo dogo ambalo na mpangilio mbovu wa machinjio hayo.

“Mkuregenzi alifika hapo na kuona  kuwa kuna udhaifu wa miondombinu ya jengo hilo na amesema waziwazi kuwa kuna ufisadi haiwezekani jengo hilo kufikia Sh. 100 milioni,” alisema Mgana.

Kubenea amesema kuwa  suala hilo atalifikisha kwenye Manispaa ili mkandarasi wa jengo hilo awajibishwe.

Akiainisha matumizi ya fedha za jimbo hilo Kwangaya amesema kuwa wametumia Sh. 75 milioni kwa ujenzi wa shule ya msingi Uzuri na Kilimani.

Pia Sh. 30 milioni kwa ujenzi wa Darasa moja la Shule ya Sekondari Manzese. Lakini pia mafuko wa jimbo hilo umekamilisha ujenzi wa wodi mbili za ghorofa za wazizi kwenye zahanati ya Manzese.

error: Content is protected !!