Saturday , 4 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba yamfukuzisha Kaze Yanga
MichezoTangulizi

Simba yamfukuzisha Kaze Yanga

Cedric Kaze, Kocha wa Yanga
Spread the love

 

MCHEZAJI wa zamani wa klabu ya Yanga, Ally Mayai amesema ubora wa kikosi cha Simba kwa sasa umechangia na kusukua, uongozi wa Yanga kumtimua kazi kocha wake, Cedric Kaze raia wa Burundi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Yanga ilifikia maamuzi ya kumfukuzisha kazi kocha huyo ambaye amedumu ndani ya kikosi hiko kwa siku 139 toka alipokuja nchini kufuatia matokeo mabovu waliopata kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara.

MwanaHALISI Online ilimtafuta Ally Mayai mchezaji wa zamani wa klabu hiyo ambaye alicheza kwa mafanikio alieleza kuwa kama Simba isingekuwa kwenye ubora na nafasi hii waliopo huwenda Yanga wasingemfukuza Kaze.

“Kama Simba isingekuwa kwenye nafasi ile, labda ingekuwa kwenye nafasi ya tisa, pengine Cedric Kaze asingefukuzwa na kusingekuwa na presha yoyote kutoka kwa mashabiki na wanachama.

“Simba kama leo hii akishinda mechi zake zote alizokuwa nazo mkononi ataiacha Yanga kwa pointi saba ndiyo sababu iliyopelekea uongozi kuondoa benchi la ufundi mara baada ya kuona kiwango cha timu kinashuka,” alisema Mayai.

Aidha Mayai aliongezea kwa kusema kuwa uwekezaji walioufanya Yanga hauendani na kiwango kinachoonekana uwanjani na hata matokeo pia kwenye michezo ya hivi karibuni.

“Yanga ilionekana kuwa na mapungufu mengi uwanjani, kiwango cha uwekezaji uliofanyika hakiakisi na matokeo ya uwanjani, kwa mfano ile mechi ya Yanga na Kengold hakukuwa na tofauti kubwa sana kati ya timu zote mbili, wakati uwekezaji uliowekezwa alitakiwa mtu aone hii ni Yanga na hii ni Kengold ambao wapo daraja la kwanza,” aliongezea mchezaji huyo wa zamani.

Uongozi wa timu hiyo umemtimua kocha huyo pamoja na benchi lake lote la ufundi huku ikiwa kileleni kwenye msimamo wakiwa na pointi 50, baada ya kucheza michezo 23, huku wapinzani wao klabu ya Simba wakiwa kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 45, na michezo 19.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!