Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kifo cha mtawa: Ni simulizi nzito
Habari Mchanganyiko

Kifo cha mtawa: Ni simulizi nzito

Agatha Yohane Mbalalila
Spread the love

 

“NAOMBA unipeleke hospitali, nimechomwa kisu,” ni kauli ya kwanza ya Agatha Yohane Mbalalila (50), mtawa wa huduma katika Kituo cha Nazaret, Ifakara mkoani Morogoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Agatha alimkimbilia Ladislaus Mloti, Katibu wa Kituo cha Nazareth, akimuomba msaada huo huku damu nyingi zikimwagika. Alimfuata kumuomba msaada wa kumkimbiza hospitali ili kuokoa maisha yake.

Kipindi hicho, hakupata nafasi ya kumuhadithia Mloti kilichomsibu, kwanza alihitaji msaada wa kupigania uhai wake.

Wakati huo, Mloti alikuwa kwenye maandalizi ya kwenda kuwanunulia nyama wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ifakara.

Mloti akiwa na mshangao kutokana na damu nyingi kumchururuzika Agatha, wakati anaanza kumsaidia, kwa nyuma alimuona muuaji akikimbizwa.

Mtu aliyekuwa akitoka mbio ni yule aliyekuwa ‘akilelewa’ na Agatha kituoni hapo, alikuwa akimkimbiza huku kisu amekishika mkononi.

Lakini nyuma ya muuaji, kulikuwa na watu wanaomkimbiza pia, baada ya muuaji kuona kundi kubwa likimkimbiza, naye alimua kujichoma kisu tumboni ili afe. Hakufa na sasa yupo hospitali chini ya ulinzi.

Mloti ambaye ni Diwani wa Mlabani anasimulia, baada ya kuona Agatha anaishiwa nguvu kutokana na kutokwa damu nyingi, yeye na wafanyakazi wenzake ‘walimzoa’ na kumuingiza kwenye gari ili kupeleka hospitali ya Rufani ya Mt. Francis.

Na kwamba, wakiwa nje wanasubiri vipimo na majibu ya vipimo vya Agatha, taarifa walizopota muda mchache baadaye ni kifo cha mtawa huyo wa Kanisa Katoliki.

Baada ya kifo hicho, anasema walitoa taarifa polisi na walipofika eneo la tukio, walimkuta mtuhumiwa akiwa amejijeruhi tumboni huku utumbo ukiwa nje na kumchukua na kumpeleka hospitali.

Mloti anasema, Agatha alianza utumishi wake kwenye kituo hicho miaka ya 90, pamoja na kwamba alikuwa muuguzi mkuu, pia alikuwa mkuu wa nyumba ya masista wa kitengo cha Amani, Ifakara.

Akizungumzia namna walivyompokea muuaji, Mloti anasema, mtu huyo alipokewa na Agatha kituoni hapo tarehe 27 Februari 2021.

Muuaji mwenyewe alijieleza, kwamba alitokea katika matibabu ya ugonjwa wa ukoma wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani. Alionesha kadi yake iliyoonesha kuwa na matatizo ya ukoma.

Kutokana na vithibitisho hivyo, alichukuliwa na kupimwa hivyo walithibitisha kuwa na tatizo hilo na kuanza kumpa matibabu mapya.

Amesema, muuaji hakuwa na na matatizo ya akili wakati akipokewa. Kilichoonekana ni kuwa, mtu huyo alikuwa na vidonda mguuni jambo ambalo liliwasukuma kuanza kumtiba vidonda hivyo.

Walichopanga, kama muuaji huyo angepona, wangemruhusu arudi nyumbani ili kuendelea na matibabu ya ukoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!