Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Simba wapungua kwa asilimia 45 Uganda
Habari Mchanganyiko

Simba wapungua kwa asilimia 45 Uganda

Spread the love

WIZARA ya utalii na wanyamapori ya Uganda imesema nchi hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa idadi ya simba kufuatia kupungua kwa asilimia 45 kwa wanyama hao katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Katika taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana Jumanne imesema idadi ya simba ilipungua kutoka 493 hadi 275, kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya binadamu na wanyamapori.

“Simba walipungua sana kutokana na mauaji ya kulipiza kisasi, yanayosababishwa na mzozo kati ya binadamu na wanyamapori,”  amesema Waziri Tom Butime alipokuwa akitoa ripoti ya utalii nchini humo.

“Idadi ya simba ilipungua kutoka 493 mwaka 2014 hadi simba 275 mwaka 2023.”

Hata hivyo, Butime alisema anafuraha kutangaza kwamba idadi ya baadhi ya viumbe imeongezeka, wakiwemo sokwe, ambao idadi ilitoka 302 mwanzoni mwa mwaka wa 2000 hadi 452 ifikapo 2022.

Uganda ina sifa ya kuwa moja ya nchi yenye viumbe vingi hai duniani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!